Na. Mwandishi Wetu,Timesmajira
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI yatembelea ofisi za TMDA Makao Makuu Dodoma kwa lengo la kujionea utendaji wa taasisi na inavyotekeleza majukumu yake.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Johannes Lukumayi amesema lengo la kamati ni kujionea kwa macho namna taasisi hii muhimu katika kulinda afya ya jamii imejipanga katika kuwahakikishia wananchi wanalindwa afya yao kupitia bidhaa za dawa na vifaa tiba.

“Tunafahamu umuhimu wa taasisi hii ndani ya nchi katika kulinda afya zetu na nje ya nchi pia katika kuongoza taasisi nyingine” amesema Lukumay.

Akichangia wakati wa kuhitimisha ziara hiyo, Adonis Bitegeko, ameipongeza Mamlaka kwa mapinduzi makubwa katika kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA na aliitaka Mamlaka kuendelea kutatua changamoto ya mifumo ya uingizaji mizigo kwa kushirikiana na wadau wengine kufuatia mabadiliko yaliyopo katika mfumo huo.
Aidha ametoa wito kwa Mamlaka kujipanga ili kuendana na ukuaji wa sayansi na Tecknolojia katika masuala ya udhibiti.
Ziara hiyo pia ilihusisha viongozi wa Wizara ya Afya akiwemo Katibu Mkuu Dkt. Seif Shekalage ambao kila mmoja aliipongeza Mamlaka kwa utendaji na namna inatekeleza majukumu yake.

More Stories
Vyuo vitano kunufaika na mradi wa UTT
Airtel Afrika Foundation yaunganisha Shule 3,296 na Intaneti
FCC,ZFCT zaimarisha ushirikiano