December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Jadon Sancho

Tetesi za soka Ulaya leo Jumatano 07.10.2020

Jadon Sancho

Klabu ya Manchester United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho, mwenye umri wa miaka 20, baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo pauni milioni 227 kutokana na dau la pauni milioni 108 linalotakiwa na Borussia Dortmund , pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake (Guardian)

West Ham walikuwa tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, mwenye umri wa miaka 22, kwa mkopo na walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la pauni 50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa. (Talksport)

Tottenham na West Ham wanapigana vikumbo kuwania saini ya beki wa kati wa Wales Joe Rodon, mwenye umri wa miaka 22, na huenda wakawasilisha ombi la dau la pauni milioni 18 kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL Oktoba 16. (Wales Online)

Klabu ya West Ham huenda ikawasilisha ombi la kumsajili beki wa Watford na timu ya Taifa ya England Craig Dawson, mwenye umri wa miaka 30, lakini watahitajika kulipa pauni milioni 4. (Sun)

Ombi la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya The hornets kutaka mkataba wa kudumu. (Manchester Evening News)

Georginio Wijnaldum

Kiungo wa kati wa Liverpool na timu ya Taifa ya Uholanzi Georginio Wijnaldum amepuuzilia mbali hamu kutoka kwa klabu ya Barcelona. Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inakamilika msimu ujao katika uwanja wa Anfield. (Mirror)

Klabu ya Saint-Etienne imeikosoa Arsenal kwa kushindwa kumruhusu beki kinda raia wa Ufaransa William Saliba kurudi katika klabu hiyo. (Talksport)

Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Uhispania Eric Garcia, mwenye umri wa miaka19, kutoka Manchester City. Barca ilitoa euro milioni 2 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Marca)

Jaribio la Barcelona kumsaini mshambuliaji wa Lyon na timu ya Taifa ya Uholanzi Memphis Depay, mwenye umri wa miaka 26, lilikatizwa baada ya winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kukataa kuondoka Manchester United. (AS)

Watford na Middlesbrough inamtaka beki wa kushoto wa Chelsea na Ghana baba Rahman , mwenye umri wa miaka 26, kwa mkopo wa muda mrefu . (Goal)

%%%%%%%%%%%%%%%