April 28, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Exim yafanya mazungumzo na wizara ya elimu kufadhili Wanafunzi elimu ya juu

Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Dodoma

KATIKA kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu nchini, timu ya Benki ya Exim ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha, Shani Kinswaga, imekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda ili kuwafadhili wanafunzi wa elimu ya juu.

Mazungumzo hayo yamefanyika Jijini Dodoma Aprili 27, 2026, lengo likiwa ni kuimarisha ushirikiano kati ya wizara hiyo na Exim, hususani katika kuwasomesha wanafunzi wanaosomea masomo ya sayansi ya data (Data Science), akili unde (Artificil Intelligence) na sayansi shirikishi.

Katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa kati, Andrew Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Stanley Kafu.