April 23, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwaselela:Waandishi wa habari muwe nguzo ya amani

Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online, Mbeya

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Ndele Mwaselela, amewataka waandishi wa habari nchini kuendelea kuwa nguzo muhimu katika kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa amani na utulivu kwa maendeleo ya taifa.

Mwaselela ametoa kauli hiyo Aprili 22, 2026, wakati akizindua kituo cha Machweo Online TV kilichopo eneo la Sokoine Jijini.

Amesema kuwa msingi mkuu wa maendeleo ya kiuchumi duniani ni uwepo wa amani na utulivu, akisisitiza kuwa vyombo vya habari vina wajibu mkubwa wa kulinda na kuendeleza tunu hiyo kwa manufaa ya taifa.

Aidha, amebainisha kuwa anatambua na kuthamini mchango wa waandishi wa habari katika kujenga jamii yenye uelewa, mshikamano na maendeleo endelevu.

Katika uzinduzi huo, Mwaselela alitoa msaada wa kamera na kompyuta mpakato (laptop) kwa Mkurugenzi wa Machweo Online TV, ikiwa ni nyenzo muhimu za kurahisisha kazi za uandishi wa habari, huku akihimiza matumizi ya teknolojia ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa habari kwa umma.

Ezekiel Kamanga ni Mkurugenzi wa Machweo Online Tv amemshukuru Mnec Mwaselela kwa kuendelea kuwa na ushirikiano na waandishi wa habari na kuhaidi kuwa chombo hicho kitazidi kuandika habari za maendeleo za mkoa wa mbeya pamoja na kuibua fursa za kiuchumi .

Kwa upande Mkurugenzi wa Mbeya yetu Online Tv ,Joseph Mwaisango amesema kuwa baadhi ya vijana wanaingia kwrnye Online kwa ajili ya tamaa kijana anaingia leo anataka afanikiwe .

“Fateni zile sheria mtaona mafanikio makubwa kazi yako itakavyokuwa nzuri ndivyo utakavyoona mafanikio makubwa yanakuja na lazima uangalie pia taarifa zako zinakuwa na ubora kiasi gani kwa wananchi wanaofatilia “amesema Mwaisango.