January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TARURA yatekeleza ahadi za Magufuli

Na Erick Mwanakulya,TimesMajira Online. Kagera

WAKALA wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), unaendelea kutetekeleza miradi ya ahadi za Rais Dkt. John Magufuli kwa kukamilisha ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilomita 2.76 kwa kiwango cha lami katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo, Meneja wa TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhandisi Dativa Telesphory amefafanua kuwa utekelezaji wa miradi ya ahadi za rais umekamilika kwa asilimia 100 baada ya ujenzi wa barabara hizo kwa kiwango cha lami kukamilika na kuanza kutumika.

“Kabla ya TARURA kuanzishwa, Wilaya ya Muleba haikuwa na lami hata mita moja lakini hadi sasa kupitia kuanzishwa kwa wakala na pia utekelezaji wa miradi ya ahadi za rais, tumetekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 2.76, ambazo zimekamilika na wananchi wameanza kunufaika na ujenzi wa barabara hizi,” amesema Mhandisi Dativa.