Na Angela Mazula, TimesMajira Online
BEKI kisiki wa klabu ya Yanga, Mghana Lamine Moro ameongeza mkataba kuwatumikia mabosi wake ambao sasa utambakiza ndani ya kikosi hicho hadi 2023.
Taarifa hizo zimethibitishwa kupitia ukurasa rasmi wa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said, ambaye amesema mchezaji huyo ataendelea kusalia Yanga hadi 2023.
Sababu za mabosi hao kumuongeza haraka Lamine mkataba ni uwezo aliouonesha katika mechi zao nne walizocheza msimu huu huku akionekana kuchangia kwa asilimia kubwa ushindi wa timu yake.
Katika mechi hizo ambazo zimewafanya Yanga kukaa katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), beki humo amefanikiwa kufunga goli mbili katika mchezo wao kwa nyumbini dhidi ya Mbeya City walioshinda goli 1-0 lakin i pia akifunga goli pekee katika mchezo wao uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar ambao pia walipata goli 1-0.
Lakini sababu nyingine za kumuongeza mkataba haraka ni taarifa za hivi karibuni ambazo zilidai kuwa mkataba wake unakaribia kufika ukingoni.
Kitendo cha uongozi Lamine Moro kuongezwa mkataba huo kimewafurahisha mashabiki wengi wa klabu ambao sasa wana uhakika kuwa mchezaji huyo ataendelea kusalia katika kikosi hicho kwa muda mrefu kwani hawana shaka na uwezo wake.
More Stories
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025
Watumishi wa Fahari wafanya Bonanza