April 23, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Sigula awatwisha zigo Walimu Wanawake juu ya malezi ya mtoto wa kike


Na Israel Mwaisaka, Rukwa

‎MBUNGE wa viti maalumu mkoa Rukwa Silvia Sigula (CCM) amewatwisha zigo Walimu Wanawake wa mkoa Rukwa kwa kuhakikisha Watoto wa kike wote wanatimiza Ndoto zao.

‎Amedai kuwa mkoa Rukwa kwa kipindi kirefu Watoto wa kike wamekua wakipitia changamoto ya kutomaliza shule kutokana na changamoto mbalimbali hivyo amewataka Walimu hao wa kike kuchukua jukumu hilo muhimu kwa kuhakikisha elimu inapewa kipaumbele kwa Watoto wa kike.

‎Hayo ameyasema leo kwenye sherehe ya kuelekea siku ya Wanawake Duniani Marchi 8,2026 iliyoandaliwa na Walimu Wanawake mkoa Rukwa kupitia (CWT) iliyofanyika leo mjini Sumbawanga katika ukumbi wa Precious Conference Centre.

‎Amesema Watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi sana lakini Walimu Wanawake wanalo jukumu la kuhakikisha wanaziondoa changamoto hizo kwa kuzikabili ili. Watoto hao wa kike waweze kupata elimu kama ilivyo kwa Watoto wa kiume itakayosaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha.

‎Walimu katika risala Yao iliyosomwa na Grace Matondwa imesema kuwa Walimu kupitia Kitengo Chao Cha Walimu Wanawake wamekua wakipigania haki zao nyingi na kuwa Sasa haki hizo zimeanza kuonekana kwa kuwepo na usawa katika mambo mengi ambayo kwa Sasa yanaonekana .

‎Awali Mwakilishi wa Wanawake CWT taifa  Elizabeth Werema alidai kuwa zilikuwepo changamoto nyingi zilizokuwa zikiwakabili Walimu wa kike na Watoto wa kike kwa ujumla lakini Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hassan amepunguza changamoto nyingi kwa kutengeneza miundo mbinu mbalimbali ya kielimu kiasi Cha mazingira ya kufundishia na kujifunzia kuwa mazuri.

‎Amesema kuwa kwa Sasa changamoto kubwa waliyonayo ni nyumba za Walimu ambapo shule nyingi Zina uhaba mkubwa wa nyumba kiasi Cha Walimu wengi hasa wa kike kupata changamoto ya kufika shuleni kwa wakati kitu kinachoweza kupunguza uwajibikaji kwao kama Walimu.

‎Walimu kwa upande wao wamehaidi  kuwa mstari wa mbele Katika suala zima la malezi kwa Watoto wote na kubwa ni kukabiliana na tatizo la Watoto wa mitaani na kuwa Walimu wanao uwezo wa kuondoa changamoto hiyo ambayo kwa sasa ni tatizo Kubwa kwa jamii.

‎Madhimisho ya siku ya Wanawake Duniani mwaka huu yamebeba ujumbe kauli mbiu isemayo”Haki na Usawa kwa Mwanamke na msichana msingi jumuishi dira 2050″