Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online -Rukwa
WAZEE wa kimila kata ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa wamemsimika rasmi Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Bazilio Mbwilo,kushika wadhifa huo baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29,2025.
Akisimikwa rasmi Februari 24,2026 na Katibu wa Baraza la Wazee wa Kimila Namanyere, Nestory Kilulu,amesema kuwa wao kama wazee wameamua kumsimika rasmi Mbunge wao kama utambuzi wa majukumu yake ya kibunge ambayo ameyaanza.
Amesema kuwa wanamkabidhi vifaa vya kimila kama fimbo,kiti na vitu vingine vya kama ishara ya ushujaa ili aweze kuwatumikia katika nafasi hiyo ya ubunge bila uoga huku wakimhadia kuwa naye wakati wa utekekalezaji majukumu yake.
Mwenyekiti wa Baraza hilo la Wazee wa Kimila,Moses Linda,amemtaka Mbunge huyo kushughulika na kero za Wananchi na kuwa wao kama wazee watampa ushirikiano.
Akizungumza mara baada ya kusimikwa rasmi Mbunge huyo wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, Bazilio Mbwilo,amesema hatawaangusha wakazi wa jimbo hilo hivyo atatekeleza kile walichomtuma.
Amesema kwa Sasa ameshafanikiwa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami mjini Namanyere na barabara za changarawe Mtenga-Matala, Mtenga-Paramawe,Kirando Korongwe,Kipili -Mkinga,Daraja Natene la Mkangale, pamoja na kuongeza vituo vya afya ambapo kwa sasa wataanza na Kata ya Mkwamba.
Pia amesema kwa sasa anaunda Vyama vya Ushirika(AMCOS) kwa kila kata na watakaojiunga watafanikiwa kukopeshwa pembejeo mbalimbali za kilimo ili kiweze kuleta tija kwa wakulima.
Diwani wa Kata ya Namanyere,Juma Masunga aliahidi kumpa ushirikiano wa Mbunge huyo na wameshaanza na baadhi ya utatuzi wa changamoto zilizopo katika kata yake.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina