March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Baba,Mama kutotekeleza majukumu chanzo familia kuvurugika

Na Mwandishi wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

MCHUNGAJI kiongozi wa Kanisa la Calvery Assembless of God,Mlima wa Nuru, Sylvester Kamala amesema familia nyingi zinatopeza mwelekeo kutokana na baba au mama kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo.

Ametoa kauli hiyo katika ibada ya jumapili iliyokuwa na lengo kubwa la uponyani wa familia kwa kauli mbiu ya “Hekima ya Ki-Mungu katika kujenga familia imara”iliyofanyika katika kanisa hilo lililopo Chamelo Nzuguni B Jijini Dodoma.

Mchungaji Kamala amesema kuwa changamoto nyingi katika familia na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili kunatokana na tabia ya baba au mama kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavya sambamba na kutokuwa na muda wa kuishirikisha familia katika masuala ya Ki-Mungu.

Amesema kuwa kitendo cha baba au mama kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavya kumesababisha kati ya familia kumi ni familia mbili ambazo zipo salama na familia nane zinakabiliana changamoto ya migogoro ya mara kwa mara.

Kiongozi huyo wa Kiroho ameeleza kuwa imefikia hatua ya baba au mama kutopata muda kabisa wa kukaa na familia na kujua changamoto zinazojitokeza jambo ambalo linachangia watoto kutokuwa na misingi imara na kukikuta zikiwa na migogoro isiyo isha.

“Kuna baba na kuna mwanaume kuma mama na kuna mwananke na siyo kila mwanaume ni baba au mwanamke ni mama,baba ni kiongoi na anatakiwa kusimamia mambo yote ya familia ikiwa ni pamoja na kusimamia barabara mambo ya Kiroho.

“Mama naye ni mlezi wa familia na ni mwangalizi wa karibu wa familia hivyo ni wajibu wake kufanya majukumu yake kwa lengo la kuifanya familia kuishi kwa amani na utulivu badala ya kumwachia dada wa kazi kufanya kazi ambazo hastahili kuzifanya kwa kisingizio kuwa dada huyo analipwa mshahara.

“Wapo akina mama ambao wamekuwa hawatambui majukumu yao na badala yake majukumu hayo wamekuwa wakiwatwisha wadada wa kazi jambo ambalo limechangia sana ndoa nyingi kuharibika na kufanya changamoto za kifamilia kushamili”ameeleza Mchungaji Kamala.

Kutokana na hali hiyo amewataka watanzaiia wote wenye familia na wale wanaotarajia kuwa na familia kujikita katika kutenda matendo mema ya Kimungu na kila mmoja kusimama katika nafasi yake ili kuzifanya familia kuwa imara jambo ambalo litasababisha kuwa na taifa la watu imara,waaminifu na watenda kazi waaminifu.