Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Mwanza
Mkoa wa Mwanza unatarajia kuadhimisha siku ya wanamke duniani kimkoa wilayani Ilemela katika uwanja wa Furahisha ambayo yatatanguliwa na kliniki ya maendeleo ya jamii Machi 4 hadi 6, 2026 Kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa, Ofisa Maendeleo ya Jamii Neema Majura,wakati wa kikao cha wadau wa maendeleo ya jamii waliokuta kwa ajili ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake Machi 8, 2026, yenye kauli mbiu “Haki na usawa kwa wanawake na wasichana msingi jumuishi kufikia Dira 2050”.

Neema,amesema maadhimisho hayo kwa mwaka 2026 yamelenga kujenga uelewa kwa jamii na wadau ili kuweza kuwekeza kwenye maendeleo jumuishi kwa kutambua haki za wananwake na wasichana.
Pia kuzifanyia kazi ili kuleta mabadiliko ya kweli kama ilivyoainishwa kwenye nguzo za Dira ya maendeleo 2050 iliyotambua umuhimu wa wanawake na wasichana kupata haki kama sehemu ya jamii


More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina