Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mwaka 1996 katikati ya chagamoto za kiafya na rasilimali chache wazo moja lilizaliwa si kwa hofu bali kwa maarifa ,huruma na udhubutu .
Kwa Sheria ya Bunge chini ya wawakilishi wa wananchi mwaka huo waliona kwamba kulikuwa na umuhimu wa kuanzisha hospital maalum kwa ajili ya kushughulikia wagonjwa wa saratani.
Hospitali ya Ocean road inatarajia kuadhimisha miaka 30 yake ikiwa na kufanya Kongamano la kwanza la Kimataifa la Saratani la Taasisi ya Saratani Ocean Road na Uzinduzi Rasmi wa Tovuti Maalum kwa Tukio hilo.
Dkt.Diwan Msema Mkurugenzi Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) anaelezea historia ya hospitali hiyo kuanzia miaka ya mwanzoni,anasema mwanzo haikuwa rahisi lakini taasisi yao ilianza safari yake kwa unyeyekevu ikiongozwa na dhamira ya isiyotikisika ya kuhudumia maisha ya watu .
Anasema miaka imeweza kusonga mbele huku taasisi hiyo iliweza kusimama na kujifunza ,kujipanua upya na kujijenga ili kukidhi mahitaji yanayobadilika ya jamii .
Msema anasema ORCI anasema imeweza kupata mafanikio makubwa sana na haya mafanikio yametokana na uwekezaji ambao Serikali imewekeza .
Anasema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kipindi cha miaka minne awamu yake ya sita aliwekeza zaidi ya shilingi millioni 40 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya matibabu ya saratani .
“Kutokana na hilo Serikali imeweza pia kuwa na wizara na Mpango mkakati wa kudhibiti saratani ambao uliisha mwaka juzi ulikuwa Mpango wa miaka 10.
“Yaani baada ya mafanikio kuonekana Ocean Road imefanikiwa, jukumu lake ilionekana ocean road peke yake haitoshi kwani Tanzania inakubwa wa takribani square mita millioni moja watu wanasafiri kilometa 1000 mpaka 1300 kuja ocean road kupatiwa matibabu,”anasema
Aidha Dkt.Msema anasema serikali iliona iwasongezee wananchi huduma karibu na maeneo wanakotoka.
Anasema kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa katika hospitali hiyo kwa sasa hakuna haja ya mgonjwa kwenda India kutafuta tiba ya saratani sababu kila kitu kinawezekekana katika hospitali yao.

Kwa upande wake Daktari Mstaafu wa Saratani,Dkt Khamza Maunda anasema kwa miaka ya nyuma hali ilikuwa ngumu kidogo kwa vifaa hasa matibabu ya saratani, kutokana na kutokuwa na wafanyakazi wa kutosha ili kuweza kutoa huduma .
Anasema pamoja na changamoto zote kitu muhimu waliweza kuishi na walikuwepo kuweza kujijenga taratibu .”Kwenye miaka ya Mwaka 2013 hadi 2018 ,Taasisi ilianzisha masomo ya kufundisha madaktari kuwa mabingwa wa kutibu magonjwa ya saratani hiki kitu kilikuwa muhimu na kimeweza kuwa msaada mkubwa kwa taasisi yetu,”anasema.
Dkt Yokebeth Vuhahula ambaye Mtaalamu wa Radiolojia anasema walikuwa hawana Idara ya Radiolojia ambayo inategemewa katika taasisi za saratani na ndo kipimo kinachokuwa kinagundua magonjwa kwa mgonjwa endapo anasaratani.
Anasema wagonjwa walkokuwa wanakuja ni lazima wawe wametokea Muhimbili ndo upelekwa katika taasisi hiyo,lakini kwa sasa wameweza kupiga hatua kutokana na kuwa na vipimo vya Pasolojia vinavyoweza kufanyika katika hospitali hiyo.

Naye Nesi Mtaalamu wa Masuala ya Onkolojia RN Mwanga Mhoka anasema
mpaka sasa mabadiliko ni makubwa katika hospitali yao na yanaonekana na hata wagonjwa wanafika wanapata huduma .
Anasema awali walikuwa na changamoto ya kuwa na idadi ya wauguzi wachache lakini kwa sasa wamekuwa na wauguzi wengi ambao wanatoa huduma kwa wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo.
Mmoja wa Balozi wa magonjwa ya Saratani ambaye ni Mshindi wa Saratani ,Babu wa kitaaa anasema matibabu na huduma zilizokuwa zinatoka kwa wauguzi katika ngazi ya chini ikiwemo ukarimu wa hali ya juu na weledi .

Anasema amegundua hospitali hiyo ni tofauti na nyingine kutoka na kuona wagonjwa ambao wanapatiwa matibabu katika hospitali hiyo ambao wamepona bado wanakuwa wanaenda katika vikao katika hospitali hiyo kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayohusu Saratani.
“Nikipogundua hilo nikaanza kuelewa tofauti ya Hospital ya ocean road ina nafasi ya kubadilisha maisha ya watu wengi ambao pengine wasiona uwezo wa kwenda nje kwa ajili ya matibabu na pia hawana uwezo Kabisa,”anasema
Dkt Carol Swai Kiongozi wa Kliniki ya Bima ya Afya anasema kutokana na uwekezaji uliofanywa na Serikali ya Tanzania kupitia Rais Dkt Samia kwa kiasi kikubwa hospitali imeweza kupiga hatua ambapo kuanzia Mwaka 2021/22 walianza kuona wateja wengi kutoka nchi za jirani hasa ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara.
Anasema wateja wamekuwa wakija kwa wingi kutokana na uwekezaji ambao umefanyika na hiyo hali imetokana na huduma kuwa rafiki na ukaribu.

More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani