Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta aina ya petroli zitakazotumika nchini hapa kuanzia Februari 4, 2026, zikionesha kushuka maradufu kwa bei ya dizeli kwa mafuta yaliyopokelewa bandari za Dar-es-Salaam, Tanga na Mtwara.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, Februari 4,2026, imebainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli,dizeli imepungua kwa shilingi 90 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar-es-Salaam, 25 kwa Tanga na shilingi 24 kwa bandari ya Mtwara.
Aidha, bei ya mafuta ya taa nayo imepungua kwa shilingi 17, 14 na 93 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia ikilinganishwa na bei za mwezi Januari 2026.
Hivyo basi, bei za rejareja za bidhaa za mafuta kwa mwezi huu, zitakuwa shilingi 2,788 kwa Dar-es-Salaam, Tanga shilingi 2,849 na Mtwara shilingi 2881 kwa bei mtawalia. Na bei ya dizeli, Dar -es+Salaam ni shilingi 2,701, Tanga 2,762 na Mtwara 2,807 huku bei ya mafuta ya taa kwa Dar-es+Salaam ikiwa ni shilingi 2,881, Tanga shilingi 2794 na Mtwara shilingi 2,838.
Aidha, kwa mwezi Februari 2026, gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar-es-Salaam ziliongezeka kwa wastani asilimia 1.88 kwa mafuta ya petroli na asilimia 1.65 kwa mafuta ya taa na kupungua kwa wastani wa asilimia 5.10 kwa mafuta
ya dizeli.
Kwa bandari ya Tanga zimepungua kwa asilimia 1.62 kwa petroli na dizeli huku bandari ya Mtwara zikipungu kwa asilimia 9.24 kwa mafuta ya petroli. Vilevile, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umeongezeka kwa asilimia 1.86.
Hata hivyo EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta nchini kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita.
Aidha,vituo vyote vya mafuta nchini vichapishe bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana kwani kutokufanya hivyo ni kosa na atakayekiuka atapata adhabu kwa mujibu wa sheria.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama