September 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BRELA yawanufaisha wakazi wa Geita katika maonesho ya tatu ya Kimataifa

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online, Geita

BRELA ni moja ya chombo Cha serikali ambacho kimepewa meno kwa mujibu wa Sheria na wanafanya shughuli zao kwa Uhuru na uweledi wa hali ya juu pasipokumuonea mtu yeyote yule.

Hivi Sasa wamejikita katika Kanda ya ziwa mkoani Geita kwenye maonyesho ya tatu ya kimaitafa yanayohusu uwekezaji wa teknolojia ya Madini ambapo na wao wameweza kushiriki kwa lengo la kutoa huduma.

Hellen Mhina yeye ni wakala msajili mkuu msaidizi wa BRELA anasema wameamua kuitikia wito wa mkoa wa kushiriki maonyesho hayo hadi sepmtemba 27 mwaka huu hivyo wananchi wamepata fursa ya kwenda kuhudumiwa.

Anasema wananchi wa mkoa wa Geita nivema wakatembelea mabanda yao ambayo yapo katika viwanja vya maonyesho hayo ili kupata huduma za usajili mbalimbali na kuhusisha taarifa zao .

Hellen anasema, wao kama Brela wameshiriki maonyesho hayo kwa lengo la kuwasogezea huduma karibu wananchi wa mkoa huo hivyo wanawaomba kufika kwenye banda lao kupata huduma.

Katika hilo wananchi kwa ujumla mkoa wa Geita anaomba wajitokeze ili kusajili wasikose nafasi hiyo muhimu na watakuwa hapo hadi kesho Semptemba 27, hivyo nivyema watanzania hususani wafanyabiashara wakajitokeza.

Anasema moja ya shughuli ambayo wanaifanya hapo ni kuhusisha taarifa za kampuni na majina ya biashara na mfanyabiashara kuhakiki taarifa zake kwa njia ya mtandao .

Msajili huyo msaidizi wa Brela anasema, usajili wa Kampuni kwasasa ni rahisi ambapo mtu anatakiwa kuwa na TIN namba , leseni ya biashara Katiba pamoja na kitambulisho cha Taifa NIDA na awe mtanzania kwa sifa hizo anauwezo wa kupata usajili bila changamoto yeyote.

Pia anasema, kama kuna mgeni na anataka usajili lazima awe na Hati ya kusafiria, katiba ya biashara, wamiliki na mtaji, huko nyuma walikuwa wanatumia mifumo ya kizamani lakini kwasasa ni mtandao tu na kila kitu kinakwenda kwa uwepesi na haraka.

Kuhusu gharama za usajili anasema, inategemea na mtaji wa wako kikubwa ni wananchi mkoani Geita na maeneo mengine nje ya mkoa husika watembelea kwenye maonyesho katika sekta hiyo ya madini na kwenye Banda la Brela na watu wanaendelea kujitokeza kwa ajili ya kusajili au kuhuisha taarifa mbalimbali.

Hata hivyo Hellen anasema, maofisa wapo wa kutosha na wanachofanya ni kupita kwenye mabanda mbalimbali kutoa elimu ya kusajili kampuni yake na faida ambayo anaweza kuipata katika kampuni ama jina la biashara yake.

Kwa upande Kaimu mkurugenzi wa Idara ya Makampuni na Majina ya Biashara kutoka Brela Mainrad Rweyemamu anasema, changamoto pia ambayo wanaipata ni pamoja na wananchi kupenda kutumia vishoka pindi wanapofanya sajili za Makampuni nakwamba kufanya hivyo ni kujichelewesha usajili.

Anasema, wao kama Brela wanakutana na changamoto wakati wakufanya sajili kutokana na mtu anayesajili kampuni wakati mwingine anakuwa si muhusika na kulazimika kumtaka muhusika jambo ambalo wakati mwingine linamchelewesha kupata usajili wake au alama ya usajili wa jina la kampuni.

Rweyemamu anasema, wanashauri wadau kuacha kutumia vishoka kwani wakati mwingine watu hawa wanaweka vizingiti kwa kuchelewesha mtu sahihi kupata usajili wake kutokana na Brela, inapohitaki nyaraka kwa wakati panajitokeza changamoto.

Anasema, hata kwenye mawasiliano wao kama Brela wanalazimika kuwasiliana mtu muhusika, kwasababu yeye ndio anakuwa amekamata usukani jambo ambalo hawakubaliani nalo hivyo wanamtaka muhusika mwenyewe ili waweze kuwasiliana nae moja kwa moja kwa maana muhusika mwenye kampuni.

Rweyemamu anasema, katika kipindi hiki Cha maonyesho ya madini mkoani Geita wananchi na zaidi wafanyabiashara wote kujitokeza kwenye viwanja vya maonyesho ya madini mkoani hapa ili kupata fursa ya kusajili kampuni yake au majina ya kampuni.

Anasema, watakuwa mkoani humo hadi semptemba 27 kwa ajili kuhakikisha wanawapatia huduma wananchi na hivyo wahakikishe wanajitokeza kwa wingi.

Anafafanua kuwa majukumu yao makubwa wao kama Brela nipamoja na kufanya usajili wa Makampuni , uandikishaji wa majina ya biashara , usajili wa alama za biashara na huduma na kutoa leseni za viwanda vikubwa Daraja A pamoja na kusajili Ataza kwa maana ubunifu.

Pia anasema, Brela imeongeza ubunifu ambapo hivi Sasa kila kitu kinafanyika kwa mtandao hivyo hakuna haja ya kubeba nyaraka mkononi kwani kila kitu kinamalizwa kwa mtanda tofauti na ilivyokuwa awali.

Anasema, pamoja na kufanya mambo hayo yote wanatoa na ushauri ambao unawawezesha wafanyabiashara kufanya biashara kwa kuzingatia uweledi na kanuni za biashara.

Anaongeza kwa kusema, muongozo wa usajili wa Kampuni kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao ni jambo la kwaza kutimiza masharti ya kufungua akaunt kwenye mfumo kwani lazima kuwa na kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA .

Kama ni BREIA kwenye kampuni lazima uwe na kitambulisho cha utaifa kutoka NiDA na namba au kitambulisho wa mlipa Kodi TIN kutoka TRA na hapo wasio watanzania wanatakiwa kuwa na Hati ya kusafiria (passport )ya nchi husika .

Kupitia Maonyesho ya madini mkoani Geita Brela unafanya kila kitu ikiwa pamoja na kupatiwa leseni kwa haraka zaidi na kila kitu kinafanyika kwa Njia ya mtandao na hata Kama awali ilitumika Njia ya kizamani na inatakiwa kuweka taarifa zako kwa mtandao wanafanya hivyo.

Rweyemamu anasema, hivi Sasa Brela kila kitu kinafanyika kwa uharaka na hakuna tena Hali ya nenda rudi Kama ilivyokuwa huko nyuma na kama Kuna mtu anakuwa na nyaraka ya mteja ameikalia kila kitu kinaoneka kwasababu mambo yote yanafanyika kwa njia ya mtandao.

Anasema, kikubwa wananchi kuepuka kutumia vishoka badala yake wao wenyewe wafike kwenye Ofisi za Brela au kwasasa wafike hapa kwenye viwanja vya maonyesho ya madini Geita watapata huduma zote na kwa haraka ilimradi atimize vigenzo.

Katika kipindi hiki cha maonyesho wananchi na wakazi wa Kanda ya ziwa katika mikoa ya Geita mwanza.shinyanga, Simiyu ,wafike kwenye maonyesho hayo kufanya usajili, kukamilisha, kuhusisha sajili zao kimtandaoa.

%%%%%%%%%%%%