Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imesema siku 100 za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha pili imepokea jumla ya Shilingi bilioni 10.5 kwa ajili ya kutoa mikopo yenye masharti nafuu na riba ya asilimia saba (7%) kwa mwaka kwa wafanyabiashara ndogondogo ambapo, tayari jumla ya Shilingi 1,351,660,000.00 zimetolewa kwa wafanyabiashara 588 kupitia mfumo wa Benki ya NMB na zoezi la utoaji mikopo linaendelea nchi nzima.
Hayo yamesemwa jijini hapa hayo leo Januari 25,2026 na Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Dorothy Gwajima wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa ahadi za Rais Samia katika siku 100 za kwanza katika uongozi wake wa kipindi cha pili cha miaka mitano ya awamu ya sita.

Dkt.Gwajima amesema katika kipindi hicho tayari Wizara hiyo imesajili jumla ya wafanyabiashara ndogondogo 119,595 katika Mfumo wa Usimamizi na usajili wa Wafanyabiashara Ndogondogo (WBN–MIS) ili waweze kunufaika na fursa za kiuchumi ambapo wanawake ni 73,341 na wanaume ni 46,254. Katika usajili huo Machinga ni 103,102, Mama na Baba Lishe ni 12,384 na Waendesha Bodaboda na Bajaj 4,109.
“Pia katika Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake, Shilingi 337,970,000 zimetolewa kwa wanawake wajasiriamali 45 kwa riba ya asilimia 4.
Pia amesema kwenye kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), jumla ya waendesha pikipiki na bajaji 209,632 wamerasimishwa kwa kupatiwa leseni za udereva.
“Hivyo zoezi la urasimishaji kwa kundi la waendesha pikipiki na bajaji linaendelea na tunahimiza wengine waendelee kujitokeza,”amesema
Katika kipindi hicho hicho Dkt.Gwajima amesema kupitia mfumo wa Wezesha Portal uliopa OWM – TAMISEMI, jumla ya vikundi 6,041 vya wajasiriamali vimetambuliwa na kusajiliwa, vikiwemo vikundi vya wanawake 3,207, vijana 2,318 na watu wenye ulemavu 516 na vikundi hivyo vina jumla ya wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali 30,205.
Vilevile amesema kupitia mfumo wa TAUSI wa ofisi hiyo, jumla ya leseni 125,621 zimetolewa kwa wajasiriamali.

Ambapo amesema usajili huo umewezesha mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri yenye thamani ya Shilingi 33,454,296,309.00 kutolewa kwa vikundi 3,776 vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kwa mchanganuo ufuatao: Vikundi vya wanawake 2,074 vimepata Shilingi 15,682,309,900.00; Vikundi vya vijana 1,357 vimepata Shilingi 16,233,093,409.00; na Vikundi vya wenye ulemavu 345 vimepata Shilingi 1,538,893,000.00.
Amezungumzia upande wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo (SIDO) amesema jumla ya wajasiriamali 16,325 (Ke 8,462 na Me 7,863) wamerasimishwa.
Pia, wajasiriamali 11,000 wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali na ujuzi wa biashara; Wajasiriamali 12,325 walipata mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji yao; na Wajasiriamali wadogo na wadogo kabisa zaidi ya 3,900 walipata namba za mlipa kodi (TIN) na leseni za biashara.
“Hivyo, hatua hizo zimechangia kuongezeka kwa kiwango cha urasimishaji, kuimarisha ajira binafsi na ajira ndogo, pamoja na kuweka msingi imara wa ukuaji wa biashara ndogo ndogo na kukua kwa mchango wake katika uchumi wa Taifa. Pia, kupitia TBS mafunzo ya uzalishaji bidhaa kwa ubora na usimamizi wa Biashara ni 1,059 na bidhaa za wajasiriamali 192 zilipewa nembo ya ubora na kuingia sokoni kwa ajili ya ushindani.
“Vilevile, huduma ya mikopo iliyotolewa na SIDO kwa wajasiriamali wadogo kuanzia tarehe 1 Novemba 2025 hadi kufikia tarehe 23 Januari, 2026 kupitia Mfuko wa Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) na kupitia Mfuko wa Dhamana ya Serikali (CGS) ni mikopo 265 yenye thamani ya 1,085,900,000 ambayo imetoa ajira 652, kati ya hizo ajira vijana ni 489,”amesema.


More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi