March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kalambo yapokea trekta ndogo za mkono 11

Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Rukwa

Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa imepokea trekta ndogo za mkono (PowerTillers) 11 kutoka Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Umwagiliaji ili kuongeza na kuimarisha upatikanaji wa huduma za zana za kilimo katika mnyororo wa uzalishaji wa mazao.

Akikabidhi zana hizo Mkuu wa Wilaya ya Kalambo,Dkt, Lazaro Komba,amesema lengo la Serikali ni kuwawezesha wakulima kuongeza uzalishaji mazao ya nafaka.

Ambapo amewaagiza Maofisa Kilimo kuweka utaratibu mzuri utakaowezesha mitambo hiyo kufanyiwa ukarabati mara kwa mara ili kuifanya kudumu kwa muda mrefu.

Dkt.Komba,amesema wakulima watazalisha kwa wakati na kwa urahisi na kuwezesha kupatikana mazao ya ziada ambayo watauza na kuchangia Halmashauri kukusanya mapato kwa wingi.

Mbunge wa Jimbo la Kalambo,Edfonce Kanoni ametumia fursa hiyo kuwataka wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo ikiwemo kushirikana na wataalam wa kilimo wakati wa kuandaaji mashamba.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Nicholas Mrango,amesema Halmashauri imeanisha maeneo yatakayofaa kujenga vituo vya zana za kilimo ikiwemo kituo cha Kata ya Matai, Lyowa na Msanzi ambapo taratibu za kuanzisha ujenzi wa vituo hivyo zinafanywa na Wizara ya Kilimo.

‘”Kwa sasa zana hizi za kilimo zitatunzwa katika maeneo yaliyoanishwa chini ya uongozi wa Serikali ya kata na vijiji kwa kushirikiana na Maofisa Kilimo na ‘Maoperator’,”amesema Mrango.