March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Airtel yatoa interneti kwa madaktari 500 waliohudhuria Mkutano

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Airtel Tanzania Imeunga mkono juhudi za sekta ya afya kwa kudhamini Mkutano wa 31 wa Mwaka wa Madaktari wa Ngozi, ulioandaliwa na Hospitali ya KCMC kupitia Idara ya Ngozi, kwa kutoa huduma ya intaneti kuanzia tarehe 7 hadi 9 Januari 2026.

Udhamini huu ni sehemu ya dhamira ya airtel kutoa huduma za intaneti zitakazo wawezesha wadau wa sekta ya afya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kurahisisha shughuli mbalimbali za kitaaluma.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Professor Daudi Rajab Mavura, Mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo cha Kanda KCMC, amethibitisha mchango wa Airtel na kuashiria athari ya huduma ya intaneti thabiti kwenye mafanikio ya mkutano.

“Tunapenda kuishukuru Airtel Tanzania kwa kutupatia huduma ya internet bure kabisa katika kipindi hiki ambapo mkutano wetu wa 31 unaokutanisha madaktari kutoka maeneo mbaklimbali, na baadhi yao wakiwa wageni hapa nchini, Hivyo huduma hii ya interneti imerahisisha mawasiliano sambamba na kurahisisha mijadala, pamoja na kuunganisha inteneti na vifaa vyetu vya mafunzo .Jambo hili limeongeza kwa kiasi kikubwa ubora wa mafunzo, mawasilisho, na ushirikiano wa kitaalamu,”amesema

Hata hivyo Airtel iliweka abanda yake katika viwanja vya mkutano huo ili kuhakikisha madaktari wanapata huduma mbalimbali, ikiwemo uwekaji wa eSIM, maonyesho ya huduma ya intaneti, usajili wa Lipa Namba, pamoja na huduma nyingine za kifedha kwa simu zilizolenga kusaidia taasisi na wataalamu wa afya.

Akizungumza kuhusu ushirikiano huo, Meneja wa kanda wa airtel, Faustin Michael Mtui, akimwakilisha mkurugenzi wa airtel Tanzania Charles Kamoto, amesema hatua hii inaonyesha dhamira ya Airtel ya kukuza maendeleo ya taifa kupitia teknolojia.

“Airtel Tanzania, tunaamini kuwa upatikanaji thabiti wa huduma za kidijitali ni kiini cha kutoa huduma bora za afya na ushirikiano wa kitaalamu.

Kwa kuunga mkono mkutano huu, tunahakikisha kwamba madaktari 500 wote waliohudhuria mkutano huu wanaweza kubadilishana maarifa bila changamoto yoyote inayohusiana na inteneti pamoja na kupata rasilimali za kidijitali.

Airtel Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kugusa taasisi mbalimbali na kusogeza huduma za kudigitali karibu na jamii. Hivyo mpango huu unaolenga kutumia teknolojia kuboresha upatikanaji, ufanisi na athari katika sekta muhimu kama afya, elimu na ujumuishaji wa kifedha.