Na Hamisi Miraji
MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imevipongeza vyombo vya habari pamoja na waandishi wake hapa nchini, kutokana na mchango wao mkubwa juu ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Pongez hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo wakati akifungua kikao kazi kilichoandaliwa na mamlaka hiyo kwa waandishi wa habari.
Lengo la kikao kazi hicho ni kutathimini mchango wa vyombo vya habari katika mapambano dhidi dawa za kulevya nchini.
Pia, kuboresha ushirikiano kati ya DCEA na vyombo vya habari kuripoti taarifa zinazohusu tatizo la dawa za kulevya ili kuongeza uelewa kwa jamii juu ya dawa za kulevya.

Kamishna Jenerali Lyimo amesema, vyombo vya habari vimekuwa na mchango mkubwa pia, kutoa elimu kwa umma, kufichua mitandao ya wahalifu kuhakikisha nchi inakuwa salama kuhusu janga hilo.
Amesema, vyombo vya habari vinapaswa kuendelea kushirikiana na taasisi za serikali na wadau wengine kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari, 0 kuhakikisha taarifa sahihi na zenye tija zinaifikia jamii kwa wakati.
“Bila ninyi hatuwezi kufanya jambo la kuwaelimisha wananchi kuhusu dawa za kulevya, kupitia vyombo vyenu vya habari ndipo Tanzania imefahamika Dunia nzima kufanikisha mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
“Awali Tanzania ilifanywa kuwa lango la dawa za kulevya, lakini sasa hilo lango limefungwa.
“Sisi Tanzania, hatutaki kuruhusu madhara ya dawa za kulevya katika Taifa letu, tunaendelea kushirikiana ili kuhakikisha dawa za ulevya zinatokomezwa,” amesema.
Aidha, amesema kupitia vyombo vya habari wananchi wanapata uelewa wa kina kuhusu mbinu ambazo wahalifu wa dawa za kulevya wanazotumia kuingiza na kusambaza dawa hizo.

Hata hivyo, Kamishna Jenerali Lyimo amesema, dawa za kuleya ni moja ya silaha hatari ambayo inaweza kushawushi ugaidi lakini pia kuua uchumi wa Taifa.
“DCEA imejulikana ndani ya nchi na nje ya nchi, kupitia makala mbalimbali na habari ambazo zimekuwa zikichapishwa kupitia vyombo habari kuwapa uelewa jamii kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya,” amesema.
Amesisitiza kuwa, ushirikiano kati ya vyombo vya habari na mamlaka ni nguzo muhimu katika kufanikisha vita hivyo, na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano, kuwajengea uelewa wa mara kwa mara.

huku akiwaomba kuhimiza jamii kuendelea kuwafichua wahalifu wa dawa za kulevya nchini.

More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani