Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Wanachi wa Mkoa wa Morogoro tayari wamejitokeza katika viwanja vya stendi ya Zamani kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za kisheria na wataalam wa Sheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Jeshi la Polisi Tanzania, Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wizara ya Ardhi, RITA na Wasaidizi wa Kisheria kutoka katika mkoa wa Morogoro wameanza kutoa huduma kwa wananchi hao.
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Juma Zuberi Homera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kliniki ya huduma za kisheria.Huduma zinazotolewa ni pamoja na utatuzi wa migogoro ya ndoa, ardhi, mirathi na ukatili wa kijinsi, huduma za uwakili, huduma za NIDA, RITA na elimu ya kisheria.

Ewe Mkaazi wa mkoa wa Morogoro na viunga vyake ambaye hujafika katika viwanja hivi hujachelewa, fika sasa ili upate huduma za Msaada wa Kisheria bila malipo.




More Stories
Mfanyabiashara,vibarua mbaroni wakituhumiwa kuchimba mahandakiÂ
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8