Ampongeza Dkt. Mwinyi kwa uwekezaji katika sekta ya Elimu.
Na Mwandishi wetu,Timesmajira
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amefungua Skuli ya Sekondari Chukwani, Zanzibar ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya Miaka 62 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Ujenzi wa skuli hiyo ambayo imegharimu shilingi bilioni 6.1 imeanzishwa kwa lengo la kuwaandaa vijana wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na
maadili, kwa kuunganisha nadharia na vitendo na hivyo kuwa na manufaa mengi ikiwemo kuongeza fursa za elimu bora kwa watoto wa Zanzibar.

Dkt. Mwigulu amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa uwekezaji mkubwa alioufanya katika sekta ya elimu.





More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI