Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linafanya uchunguzi ili kubaini mtu au watu waliohusika na mauaji ya Evans
Mohamed (51) ambaye dereva wa gari na mkazi wa mtaa wa Mnyampala, Kata ya Nyamanoro wilayani Ilemela mkoani hapa.
Ambapo inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Januari Mosi,2026, majira ya
saa 1.00 asubuhi mtaa wa Kileleni, Kata ya Kitangiri wilayani Ilemela.
Akizungumza jijini hapa Januari 3,2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbord Mutafungwa,ameleza kuwa
marehemu aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali usoni na kichwani na mtu au watu ambao bado hawajafahamika.
Mutafungwa amesema kuwa mwili wa marehemu huyo ulikutwa katika mtaa huo wa Kileleni, ulichukuliwa na Askari Polisi na kupelekwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure na kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu.
“Baada ya uchunguzi Januari 2,2026
walikabidhiwa ndugu kwa taratibu za mazishi.Tunaendelea na uchunguzi
wa kina ili kuwabaini wahusika na kubaini mazingira ya tukio hili la mauaji na hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wahusika,”amesema Mutafungwa.
Hivyo ametoa wito kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kufanikisha uchunguzi huo wawasilishe kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili zifanyiwe kazi kwa haraka na
wahalifu wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi