Na Mwandishi wetu,Timesmajira
SERIKALI imewataka wamiliki wa maeneo ya kazi nchini ambao maeneo yao hayasajiliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pakazi (OSHA) kusajili maeneo hayo ndani ya siku tisini kuanzia Januari 2026.
Agizo Hilo la Serikali limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano,Deus Sangu alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za QSHA zilizopo Kinondoni jijini Dar es salaam.
Ziara hiyo ambayo ni ya Kwanza kwa Taasisi ya OSHA yangu waziri huyo alipoteuliwa na Rais Dkt. Samia suluhu Hassani kusimamia masuala ya kazi nchini imelenga kujifunza jinsi OSHA pamoja na Taasisi nyingine chini ya wizara yake zinavyotekeleza majukumu yake.
Akizungumza na menejimenti na watumishi wa OSHA Waziri Sangu amesema Taasisi ya OSHA inayodhamana kubwa ya kulinda nguvu kazi ya Taifa dhidi ya ajali, Magonjwa na vifo vitokanavyo na mazingira ya kazi yasiyokuwa rafiki.
Aidha Waziri Sangu amesema Ili OSHA iweze kusimamia ipasavyo uzingatiaji wa kanuni bora za Usalama na Afya Mahali pakazi nchini, maeneo hayo yanapaswa kutambulika na OSHA kupitia kusajili.
Aidha Waziri huyo amewataka Watumishi wa OSHA kufanya kazi kwa bidii, kujituma kuzingatia weledi Katika kuwawezesha waajiri hao kuzingatia ushauri ambao kumekuwa ukitolewa na wataalamu wa OSHA.
” Usajili wa sehemu za kazi nchini ni kwa mujibu wa kifungu cha 16 na 17 cha Sheria ya usalama na Afya Mahali pakazi ya mwaka 2003 ambapo OSHA husajiri maeneo ya kazi na kisha na huyafikia kwa ajili ya ukaguzi na ushauri wa kitaalamu juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi,”” ameeleza Waziri Sangu
Akitoa maelekezo kuhusu taasisi ya OSHA kwa waziri, Mtendaji Mkuu wa OSHA Khadija Mwenda amesema yeye na watumishi wa OSHA wamefarijika kumpokea waziri na ujumbe wake ambapo watakuwa tayari kupokea maelekezo yote ya Serikali na kuyafanyia kazi ipasavyo.
” Kwa niaba ya watumishi wenzangu nikuhikikishie kwamba hatutakubali kuwa sababu ya kukwamisha utendaji wenu Bali tutajitahidi kutekeleza majukumu yetu ipasavyo na hivyo kuwafanya nyinyi viongozi wetu kifua mbele kutokana na utendaji wetu mziri,” ameeleza kiongozi mkuu wa Taasisi ya OSHA Mwenda.
Waziri Sangu ameambatana na Naibu wake, Rahma Kisuo pamoja na kamishna wa kazi Suzan Mkangwa ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
OSHA ni taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ( Kazi Ajira na Mahusiano) yenye jukumu lakutoa na kusimamia miongozo ya Usalama na Afya Mahali pakazi ambapo katika kutekeleza majukumu ya kusajilia maeneo ya kazi na kuyafikia kwa ajili ukaguzi na ushauri wa kitaalamu juu ya uboreshaji wa mazingira ya kazi.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako