Na. Israel Mwaisaka, Timesmajira Online -Rukwa
Serikali imesema itaanzisha kitengo maalum cha huduma kitakachofanya kazi kwa saa 24 chenye jukumu la kupokea, kusikiliza, kufanyia kazi maoni, mapendekezo pamoja na kero za wananchi.
Kitengo hicho kitawezesha wananchi kuwasilisha changamoto zao moja kwa moja bila vikwazo kwa kusaidia Serikali kupata mrejesho wa haraka kwa ajili ya kuboresha sera na huduma.
Hayo yameelezwa Desemba 23, 2025 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano,Deus Sangu,mkoani Rukwa alipofanya kikao na wadau wa mahusiano kutoka makundi ya kijamii, kisiasa, kiuchumi na wawakilishi wa kundi la vijana.
Sangu,amesisitiza umuhimu wa mawasiliano na uwajibikaji kati ya Serikali na wananchi kwa ajili ya kuimarisha imani, mshikamano wa kitaifa na maendeleo jumuishi.
‎Amesema lengo la kikao ni kutambulisha shughuli za ofisi yake na kutekekeza mkakati wa kuwafikia wadau wa mahusiano ili kujenga uelewa wa pamoja kwa maendeleo ya taifa.
Kikao hicho kimeongozwa na kauli mbiu isemayo “Mahusiano imara,msingi wa mshikamo wa taifa.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi