March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Polisi Mwanza yaendelea kuimarisha usalama  kuelekea Krismasi na mwaka mpya

Judith Ferdinand, Timesmajira Online-Mwanza

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama,limeendelea kuimarisha mifumo ya kiusalama maeneo yote  katika kuelekea siku za mwisho wa mwaka ikiwemo Krismasi(Christmas) na mwaka mpya.

Pamoja na kuchukua hatua za haraka za kisheria kwa watu wanaojihusisha na uhalifu wa makosa ya jinai na ya usalama barabarani.

Akizungumza Desemba 24,2025 na waandishi wa habari mkoani hapa,Kamanda Mkoa wa Mwanza Wilbord Mutafungwa,amesema jeshi hilo linaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa amani.

Sambamba na kufanya doria,misako na oparesheninkwa lengo la kuzuia na kudhibiti vitendo vya uhalifu kutokana na  matishio ya uwepo wa maandamano wanayoyasikia kuratibiwa kupitia mitandao ya kijamii kuelekea sherehe za mwisho wa mwaka za Krismasi na mwaka mpya wa 2026.

“Wananchi wasiwe na hofu kwani kupitia mpango kazi tayari tumejipanga vizuri askari wapo maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote kwa kushirikiana na wananchi,”amesema Mutafungwa na kuongeza:

“Kutokana na ushirikiano huo tutahakikisha hakuna kundi au mtu yeyote atakaye pewa nafasi ya kuvuruga amani katika kipindi hiki cha sikukuu na baada ya sikukuu,”.

Sanjari na hayo Mutafungwa ametoa tahadhari ya usalama wakati na baada ya  sikukuu hizo kwa kuwataka wananchi kuendelea kutunza amani kwa kila mmoja kutiki sheria na kutoa taarifa endapo ataona na  viashiria vyovyote vya uhalifu  kwa viongozi wa serikali katika maeneo yao,polisi au vyombo vingine vya usalama.

“Endapo familia itawalazimi kwenda kusherekea sikukuu hizi nje ya mazingira ya nyumba zao,wasiache maeneo yao bila uangalizi.Wazazo wasiwaruhisi watoto kwenda matembezi au maeny ya burudani bila kuwa na uangaliy wa watu wazima,”amesema Mutafungwa.

Pia ametoa onyo kwa wenye nyumba na kumbi za starehe kuhakikisha wanachukua tahadhari zote za liusala kwa mujibu wa leseni zao na hakuna kuandaa au kuendesha disko toto.