March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madiwani Ilala watakiwa kushirikiana na Wenyeviti wa mitaa

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Ilala

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar-es-Salaam, kufanya kazi kwa kushirikiana na Watendaji na Wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi

Mpogolo, amrsema hayo wilayani Ilala ,wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam.

“Nawaomba Madiwani wangu wa Halmashauri ya Jiji mkawe kiunganishi baina yenu na Watendaji pamoja na Wenyeviti wa Serikali za mitaa,katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ili tumsaidie Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan,”amesema Mpogolo.

Pia amewataka Madiwani kushuka chini ngazi ya mtaa kwa kushirikiana na watendaji na Wenyeviti ndio kwenye kero kubwa kwa kuweka vikao vya utatuzi wa kero na mikutano ya wananchi.

Sanjari na hayo amewataka kutumia mafunzo kwa tija kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika maeneo yao kwani wakifahamu shida za wananchi hawawezi kuona mzigo kuwahudumia.

Aidha amewataka Madiwani hao kusimamia ukusanyaji mapato ya Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam ili Serikali iweze kufikia malengo pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kuu