Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Sikonge
Madiwani na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora,wametakiwa kwenda na kasi ya serikali katika kukusanya mapato ili kuharakisha maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmasahauri ya Wilaya ya Sikonge,Andrea Gasto,ametoa rai hiyo wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kuchaguliwa kuongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo 2025-2030.

Amesema kuwa wakazi wa halmashauri hiyo wana imani na matumaini makubwa na Madiwani na Watumishi wa halmashauri hiyo na wako tayari kuwapa ushirikiano ili kuchocheo kasi ya maendeleo yao.
Amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameishatoa mwelekeo wa yale atakayowafanyia wana Sikonge ndani ya siku 100 za mwanzo na mengineyo mengi kama yalivyobainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025-2030.
“Wakazi wa Sikonge wana imani na serikali naomba kila mmoja aliyepewa dhamana ya kusimamia maendeleo yao afanye kazi kwa bidii na moyo wa dhati,”amesema.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Sikonge,Thomas Myinga,amewataka madiwani na wataalamu kuwa karibu na wananchi, kusikiliza kero zao,kuzitafutia ufumbuzi na kuwaeleza umuhimu wa miradi inayotekelezwa na serikali.

Amewataka kusimamia suala zima la ukusanyaji mapato katika maeneo yao ili kuongeza mapato ya halmashauri na kuchochea kasi ya utekelezaji miradi ya maendeleo ndani ya kata zao.
Aidha amemwagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Seleman Pandawe kuhakikisha miradi ya nyuma yote inatengewa fedha katika bajeti ya mwaka huu ili utekelezaji wake uendelee na kuwanufaisha wananchi.

More Stories
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10