Na Mwandishi wetu,Timesmajira
TAASISI ya Fadhii Teens imezindua mradi maalumu unaojihusisha na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya watoto na vijana mashuleni.
Mradi huo wenye lengo la kuisaidia jamii katika upatikanaji wa elimu bora kwenye baadhi ya makundi yaliyo kuwa na changamoto mbalimbali zikiwemo umasikini na kutengwa.
Akizindua mradi huo jijini Dar es salaam Mratibu wa Mradi wa asasi hiyo, Anitha Modesti amesema kuwa ni kwa namna gani watoto wanaweza kushiriki katika masomo yao mashuleni, ambapo alidai kwamba ni vema kuvishirisha vyombo vya habari katika kutoa elimu ingawa wazazi wanawajibu mkubwa kwa vijana hao.

“Kupitia vyombo vya habari hususani vipindi mbambali vya redio watoto na wazazi wataweza kusikia namna bora na kipekee kwa mtoto kuweza kuhudhuria masomo mashuleni,, amesema Anitha
Aidha Mratibu huyo amesema kuwa Kuna namna bora ya kumwezesha mtoto kufanikisha matarajio yake ambapo ni pamoja na kumsimamia kidhati kwa ajili manufaa yake ya sasa na ya baadae.

Katika huo mjadala vilielezwa vikwazo mbalimbali vinavyopelekea watoto kushindwa kuhudhuria masomo mashuleni ikiwemo suala la umasikini, makundi rika,kutokujua kusoma na kuandika sambamba na ndoa za utotoniHata hivyo asasi hiyo imekuja na suluhu kwa walimu kuwa pamoja na wazazi kushiriki katika kuwezesha wanafunzi wanakuwa msfari wa mbele katika maendeleo ya watoto kuhudhuria masomo kwa nyakati zote.
Juhudi za kipekee kwa wazazi na walimu kuweza kushirikshwa Katika midaharo mbalimbali Ili kutambua majukumu yao dhidi ya malezi bora kwa watoto wao na kutambua ndoto za vijana wab ni fursa pekee kwa maisha yao ya baadaeni.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI