March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mixx yazindua Kampeni kubwa mwisho wa mwaka

Na Hamis Miraji,Timesmajira Online

MIXXimezindua kampeni kubwa ya mwisho wa mwaka – Magift ya Mixx Pesa, ikiwa ni shukrani kwa wateja wanaoendelea kuichagua Mixx, kila siku.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni hiyo jana, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx, Angelica Pesha alisema katika msimu huu wa sikukuu wenye mahitaji mengi.

Amesema, Mixx imekuja na zawadi nono kupitia kila muamala, ikiwemo milioni 1 kila siku, milioni 5 kila wiki, ushindi wa milioni 10 MixxMas,lakini pia, na mwaka mpya na Jackpot ya milioni 50 mwishoni mwa kampeni.

“Kampeni hii ni uthibitisho wa jinsi tunavyothamini uaminifu wa wateja wetu na dhamira ya kuendelea kubuni huduma rahisi, nafuu na zinazowawezesha katika malipo, akiba na mahitaji yote ya kifedha.

*Tunawaalika wateja wote kutumia huduma zetu za wakala, Mixx Super App au *150*01# ili kupata nafasi ya kushinda na kuufunga mwaka kwa nguvu kupitia “Magift ya Mixx Pesa,” amesema Pesha