Na Mwandishi Wetu,Timesmajira
YAs imethibitisha kuendelea kushirikiana na waandaaji wa Korosho Marathon 2025, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha wakulima wa korosho na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi mkoani Mtwara kupitia michezo.
Hayo yamejiri wakati wa hafla ya kufunga mbio za Korosho Marathon zilizofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Millenium Beach mkoani Mtwara.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Maendeleo ya Vijana), Dkt. Joel Nanauka, aliipongeza Yas kwa mchango wake katika kuboresha ustawi wa vijana, wakulima na jamii ya Mtwara.
“Niwapongeze sana Yas kwa uwekezaji mkubwa mnaoufanya katika mkoa wa Mtwara, kuanzia miundombinu ya mawasiliano, huduma za kifedha kwa wakulima, hadi ushiriki wenu katika matukio kama Korosho Marathon.
Haya ni matokeo ya kampuni inayotazama mbali na inayotambua kwamba maendeleo ya taifa letu yanategemea uwezeshaji wa vijana, wakulima na familia zetu.

Serikali itaendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha wakulima wa korosho wanapata huduma bora, salama na za uhakika.”
Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Pwani Kusini, Fadhila Saidi amesema ushiriki wa Yas na Mixx katika Korosho Marathon ni sehemu ya mkakati wa kampuni kuboresha maisha ya wakulima na jamii kupitia huduma bunifu za kidijitali, kifedha na kijamii.
Kupitia huduma zake, Yas na Mixx zimeendelea kuwa washirika muhimu wa maendeleo ya mkoa wa Mtwara, ikiwemo: Kuwezesha malipo kidijitali kwa kaya maskini kwa kushirikiana na TASAF na Halmashauri ya Mkoa.Kupanua upatikanaji wa mtandao wa 4G katika kata zote na 5G Mtwara Mjini.
Ushirikiano na Bodi ya Korosho, AMCOS na vyama vikuu vya Ushirika kuwezesha malipo ya wakulima kupitia Mixx kwa haraka na kwa usalama zaidi.
Kutoa mikopo ya riba nafuu, bima ya afya na huduma nyingine za kifedha kuongeza tija ya wakulima.Kuwezesha zaidi ya shilingi bilioni 150 kulipwa kwa wakulima zaidi ya laki moja tangu mwaka 2017.

Kudhamini matukio ya kijamii na Serikali kama Nyangumi Festival na Msanga Mkuu Festival, huku kisisitiza umuhimu wa mashindano haya, Saidi amesema:
“Korosho Marathon siyo tu tukio la michezo, bali ni jukwaa muhimu la kuutangaza mkoa wa Mtwara kimataifa, kukuza utalii, biashara, afya na umoja wa jamii. Ni ishara ya fahari ya wakulima na mchango wao katika uchumi wa Taifa.”
Ameongeza kuwa, Yas itaendelea kushirikiana na waandaaji wa mashindano kuhakikisha mbio hizi zinakua kwa ukubwa, ushawishi na manufaa kwa vikundi vya vijana, wakulima na jamii kwa ujumla na kuwataka wadau wa maendeleo kuendelea kuunga mkono mashindano haya ili kuimarisha mustakabali wa wakulima na kuleta maendeleo endelevu katika mkoa wa Mtwara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Korosho Marathon, Ndugu Nelson Mrashani, amemshukuru Dkt. Nanauka kwa kushirika katika mbio hizo na vilevile aliwapongeza washindi na kuwashukuru washirika wa mbio
“Tunawashukuru sana washirika wetu na wakimbiaji wote kwa kuungana nasi katika juhudi za kuchochea Michezo, Afya na Biashara hapa Mtwara alisema Mrashani.

“Washindi wa Korosho International Marathon 2025 ni pamoja na; -Washindi wa Km 21 – Wanawake1. Cecilia Ginoka- ameshinda milioni 3.52, Vaileth Adam – ameshinda milioni 2.53, Natalia Sule – ameshinda milioni 2.
Washindi Km 21 – Wanaume1. Peter Gidoska- ameshinda milioni 3.52, Protas Kableni ameshinda milioni 2.53, Dickson Paul ameshinda milioni 2.
Washindi wa Km 10 wanawake1. Grace Jackson Charles ameshinda milioni 22, Enestina Ngoloje ameshinda milioni 1.53, Deborah Benedict ameshinda milioni 1.
Washindi wa Km 10 wanaume1. Jumanne Mnada ameshinda milioni 22, John Joseph ameshinda milioni 1.53, Shedrack Damas – ameshinda milioni 1.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI