March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chama cha Maofisa uhusiano waomba kushirikishwa kwenye miradi

Na Queen Lema,Timesmajiraonline,Arusha

CHAMA Cha Maofisa Uhusiano Tanzania kimeiomba Serikali pamoja sekta binafsi kuhakikisha zinawashirikisha wana taaluma katika sekta ya mahusiano kwenye miradi mbalimbali ili kurahisisha mambo mbalimbali ikiwemo ufuatiliaji na utoaji wa taarifa.

Ombo hilo limetolewa jijini hapa Novemba 28,2025 na mwanzilishi wa Chama hicho  nchini Loti Makuza wakati akiongea kwenye kongamano la maafisa habari kutoka Afrika Mashariki.

Loti amesema kuwa sekta ya mahusiano ni moja ya sekta muhimu hivyo inapaswa kupewa kipaumbele lakini hata ushirikishwaji kwa maafisa uhusiano hasa kwenye mikakati na utekelezaji wa jambo lolote.

“Kwa sasa miradi mbalimbali inatakiwa kusemewa vyema na maafisa uhusiano wanapokuwa na taarifa kamili inarahisisha kifanya hivyo kwa usahihi,

“Ndugu wanahabari haileti picha wewe ni Afisa habari unaulizwa swali kuhusiana na taasisi yako au shirika lako unakosa jibu na kusema ngoja nikaulize mabosi wako”amesema Loti.

Naye Gilbert Kinono kutoka kampuni ya usafiri wa mtandaoni Bolt ambaye ndiye mtoa mada mkuu amesema kuwa Bolt ni huduma ambayo imekuwa msadaa mkubwa sana kwa kuwa watanzania wameweza kunufaika na kupata ajira

Amesema kuwa katika kongamano hilo wao BOLT pamoja na dhima hiyo ya kujenga uaminifu kwa wananchi pia wamelenga pamoja na kuleza wazi wazi dhima ya kampuni ya Bolt katika kuchochea mandeleo ya nchi sambamba na kuzalisha ajira mpya.