Na Mwandishi wetu
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mashujaa wa Ulinzi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Morogoro, Shujaa Joyce Hamis Nyangi, ameshiriki mahafali ya kidini ya Chuo cha FDC Ilonga, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa CASFETA na UKWATA.
Katika tukio hilo lenye heshima kubwa, Shujaa Joyce aliambatana na mashujaa wenzake watatu Peace Kajei, Mama Seyeye, na Mwenyekiti wa Mkoa wa Morogoro wa Makada Walimu, Shujaa Shoni, Wote kwa pamoja waliwatia moyo wanafunzi na vijana kwa ujumla kujiepusha na vitendo viovu vinavyoweza kuhatarisha maadili na mustakabali wa maisha yao.
Akiwa mgeni rasmi, Shujaa Joyce aliendesha mafunzo maalum kuhusu ukatili wa kijinsia, akifafanua maana yake, aina mbalimbali za ukatili, namna ya kuripoti matukio hayo, na mbinu za kuepuka vitendo hivyo.
Alisisitiza umuhimu wa kuilinda amani ya nchi, huku akiwahimiza vijana kutoa taarifa mapema kwa vyombo husika endapo wataona viashiria vya uvunjifu wa amani.
Aidha, katika kuonyesha mfano wa moyo wa kujitolea, Shujaa Joyce alichangia mahitaji ya kidini kwa wanachuo, akishirikiana na waalikwa wengine katika kufanikisha tukio hilo.
Alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa chuo, walimu, wafanyakazi, na viongozi wote wa CASFETA na UKWATA kwa ukarimu na ushirikiano wao wa hali ya juu.

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi