March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwanasheria Mkuu wa Serikali aapishwa

Na Mwandishi Wetu

RAIS Samia Suluhu Hassan amemwapisha Hamza Johari kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Johari aliapishwa jana Novemba 5, 20254, Ikulu ya Chamwino, jijini Dodoma ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali.

Miongoni mwa viongozi hao ni Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi. Johari ateuliwa na Rais Samia Novemba 3, 2025 baada ya Samia kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya MuunganoTanzania.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa Johari aliahidi kutekeleza majukumu yake na kufanya uamuzi kwa kufuata Katiba, sheria, kanuni, taratibu, mila na desturi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Sitatoa shinikizo linalokiuka sheria, kanuni, taratibu na miongozo katika utendaji kazi za umma,” alisema Johari.

Johari anaendelea na wadhifa huo baada ya kuwa kuteuliwa kwa mara ya kwanza Agosti 15, 2024 kuchukua nafasi ya Dkt. Eliezer Feleshi ambaye aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Kabla ya uteuzi huo, Johari alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

Rais Samia alimteua Johari saa chache baada ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Masaju katika sherehe zilifanyikia Uwanja wa Gwaride, Ikulu ya Chamwino.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ilimtangaza Samia mshindi wa urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 kwa kupata kura asilimia 97.6 ya kura halali zaidi ya milioni 32 zilizopigwa.

Mwishooooooo