Na Judith Ferdinand, Timesmajira Online – Mwanza
Mgombea wa kiti urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufunga kampeni za chama hicho,ambayo inafanyika kwa Kanda ya Ziwa Oktoba 28, 2025,uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza, siku moja kabla ya zoezi la kupiga kura litakalofanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Oktoba 26, 2025, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Omary Mtuwa, amesema chama kimeamua kufungia kampeni Kanda ya Ziwa kutokana na umuhimu wa kanda hiyo katika mchango wake wa kisiasa na kiuchumi kwa taifa.
“Mwanza ni sura ya Kanda ya Ziwa, na zaidi ya asilimia 100 ya wakazi wake wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za uzalishaji kama uvuvi, kilimo na biashara. Hivyo tumeamua kufungia kampeni zetu hapa ili kuonesha heshima hiyo,” amesema Mtuwa.
Mtuwa ameeleza kuwa Kanda ya Ziwa inakadiriwa kuwa na takribani asilimia 38 ya wapiga kura wote nchini, huku Mkoa wa Mwanza ukiwa na zaidi ya wapiga kura milioni mbili,hivyo lengo chama hicho ni kuhakikisha kinapata angalau asilimia 50 ya kura kutoka mkoa huo na kanda nzima.
“Tunataka kuona mgombea wetu anapata angalau nusu ya kura kutoka Mwanza na Kanda ya Ziwa. Hii ni sehemu muhimu kwa ushindi wa CCM kitaifa,” amesema Mtuwa.
Mtuwa ameongeza kuwa mkutano wa kufunga kampeni utakuwa wa kisayansi, ambapo kutakuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa nda
Amesema chama kinachotaka kushika dola ni lazima kijiweke karibu na wananchi na kufanya kampeni kwa mujibu wa sheria, kwa kuweka mabango, mikutano na matangazo ya kumtambulisha mgombea wake ambapo CCM pia imefanya hivyo.
Sanjari na hayo amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kujitokeza siku ya Oktoba 28,mwaka huu katika ufungaji wa kampeni pia Serikali ya CCM imejipanga kulinda usalama wa wananchi hadi siku ya uchaguzi.
“Mkutano utakuwa wa amani, na chama kimejipanga kuhakikisha usalama na ulinzi wa wananchi unaimarishwa,hivyo wananchi jitokezeni kwa wingi ili kumaliza kampeni hizo kwa kishindo,”amesema Mtuwa.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako