Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya mawasiliano ya Yas, imezidi kuonyesha dhamira yake ya kuchochea maendeleo ya elimu ya teknolojia nchini, baada ya kufunga huduma ya intaneti yenye kasi katika Shule ya Sekondari Butiama, mkoani Mara.
Lengo ni kuwawezesha wanafunzi kujifunza somo la TEHAMA na kompyuta kwa ufanisi zaidi.
Akizungumza katika mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo, Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Ziwa, Joseph Mtalemwa amesema mradi huo ni sehemu ya juhudi endelevu za Kampuni hiyo kuinua elimu ya teknolojia katika shule za vijijini na kuwaandaa wanafunzi kukabiliana na ulimwengu wa kidijitali.

“Tunatambua kwamba dunia ya leo inaongozwa na teknolojia. Ndiyo maana tumeamua kuhakikisha shule kama Butiama zinapata intaneti ya kasi, ili wanafunzi waweze kupata maarifa mapya na kujifunza kwa njia za kisasa,” amesema Mtalemwa.
Wanafunzi wa Butiama walieleza furaha yao kutokana na msaada huo, wakisema huduma hiyo ya intaneti itawarahisishia kufanya utafiti, kujifunza kwa njia ya mtandao.
Pia, kuongeza uelewa wao katika masomo mbalimbali. Waliahidi kutumia fursa hiyo kusoma kwa bidii na kupata matokeo bora kama njia ya kuthamini mchango wa Yas.

Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Shule ya Butiaama, Teddy Denya ameishukuru Yas kwa hatua hiyo, huku akisema imefungua ukurasa mpya katika ufundishaji wa masomo ya TEHAMA na kompyuta shuleni hapo.
“Huduma hii si msaada tu bali ni uwekezaji katika elimu ya vijana wetu.
“Itasaidia walimu kufundisha kwa ufanisi zaidi na wanafunzi kuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira la sasa,” amesema Denya.
Kupitia miradi kama hiyo, Yas inaendelea kujikita katika kuinua ustawi wa jamii kupitia teknolojia.
Pia, ikilenga kufikisha huduma zake za mawasiliano na intaneti hadi maeneo ya pembezoni ili kuhakikisha Watanzania wote wananufaika na mapinduzi ya kidijitali.


More Stories
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi
Waziri Mkuu kuanza ziara mkoani Rukwa Marchi 8 Hadi 10
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani