Na Esther Macha Timesmajira Online, Mbeya
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Suma Fyandomo, ameendelea na kampeni ya mguu kwa mguu kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa kushiriki katika uchaguzi mkuu Oktoba 29, 2025 na kuchagua wagombea wa chama hicho.
Fyandomo ameshirikiana na wagombea wa nafasi za Ubunge wa chama hicho wa majimbo yote mkoani humo, akiwahimiza wananchi umuhimu wa kuchagua viongozi wanaotokana na CCM.

Amekuwa akizungumza na wananchi moja kwa moja kwa kuwafuata katika maeneo yao ikiwemo sokoni, vijiweni, kwenye maduka ya nyama, saluni za kike, gereji, vilabu vya pombe za kienyeji pamoja na wajasiriamali wadogo.
Ambapo ametumia fursa hiyo kuwaelezea wananchi hao namna ilani ya uchaguzi ya CCM 2020–2025 iliyotekelezwa na malengo mapya kuelekea ilani ya 2025–2030.
“Tunaona maendeleo yaliyofanywa na Serikali chini ya CCM katika sekta za afya, maji, barabara, elimu na nishati vijijini na mijini,”.
Hivyo amewaomba wananchi hao kumpigia kura Dkt Samia Suluhu Hassan kwa nafasi ya urais, wabunge na madiwani wanaotokana na CCM na kuwataka kutokubali kurubuniwa na maneno ya chuki.
Pia Fyandomo, amewahimiza wananchi kudumisha amani na mshikamano ikiwemo wanawake na vijana, madereva wa bodaboda, bajaji, mama lishe na baba lishe.


More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi