March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea Ubunge  kupitia CUF aahidi kukomesha  ubadilifu 

Na Mwandishi Wetu Timesmajira Online-Tabora

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya chama cha Wananchi CUF,Kapasha Haji Kapasha,ameomba wananchi  wa Jimbo hilo kumpigia kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu,ili aweze  kukomeshe vitendo vya ubadhirifu wa mali za umma.

Kapasha ameahidi hayo wakati wa mkutano wake wa kampeni uliofanyika  uwanja wa taasisi, eneo la Soko Kuu Mjini hapa,ambapo amesema  rasilimali nyingi za umma zimekuwa haziwanufaishi wananchi kutokana na usimamizi mbovu,ambao umesababisha Halmashauri ya Manispaa ya Tabora kupoteza mapato mengi, hivyo akaahidi kuwa kama atapata ridhaa ya kuwa Mbunge wao atayasimamia ipasavyo.

“Kama nitapata ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hili,ndani ya siku 100 za kwanza nitahakikisha mali zote za Manispaa  zilizoibiwa au kumilikishwa kwa watu wengine zinarejeshwa haraka iwezekanavyo,”amesema Kashapa na kuongeza:

“Msifanye makosa, naomba mnichague kuwa Mbunge bunge wa Jimbo hili Oktoba 29 mwaka huu,ili nikawatetee bungeni na kuchochea mabadiliko ya kiutendaji katika halmashauri zetu kwani  mambo mengi yanafanyika ovyo,”.

Sanjari na hayo amesema,viongozi wengi wanaochaguliwa wamekuwa wakifumbia macho mambo ya msingi ikiwemo kero za wananchi hali inayosababisha kushindwa kutatuliwa na kuongeza malalamiko zaidi.

Hata hivyo amesema,chama hicho kipo kwa ajili ya kutetea haki za wananchi hivyo amewahimiza kumchagua mgombea wa kiti cha Urais kupitia CUF,Gombo Samandito na wagombea Ubunge na Udiwani  kwani hawatajuta.

Kwa upande wake mgombea Udiwani wa CUF  Kata ya Chemchem,Nunu  Ally,amesema Kata hiyo ipo nyuma kimaendeleo hivyo amewaomba wananchi wamoe ridhaa ya kuwa Diwani ili akasimamie maendeleo.