Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Kilwa
Chama Cha Mapinduzi(CCM), kimesema endapo kitapata ridhaa kwa mara nyingine kushika dola,kimedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo kwa kuendelea utaratibu wa kutoa mbolea ya ruzuku.
Uendelezaji wa miche bora ya korosho ili wakulima waipate na kufanya kilimo chenye tija katika zao hilo pamoja na kujenga ghala la kuhifadhia nataka.
Pia Serikali chini ya CCM kwa miaka mitano ijayo endapo itashinda katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29,2025,itashirikiana na Bodi ya Korosho na Bodi za Mazao, kuhakikisha bei za mazao hayo zinaendelea kuwa nzuri na rafiki kwa wakulima na wanunuzi.

Hayo yameelezwa na Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia CCM,Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi,Oktoba 20, 2025 kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kata ya Tingi, Kilwa Kaskazini.
Ambapo amesema,ili wakulima walime kitaalamu, Serikali ya chama hicho itaimarisha mashamba darasa na uboreshwaji wa miundombinu ya umwagiliaji.
Dkt.Nchimbi amesema,katika sekta ya uvuvi kupitia ilani ya CCM ya miaka mitano ya 2025-2030, watakamilisha bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko,kujenga soko la kisasa la samaki pamoja na majokofu.
Sanjari na hayo amesema,mgombea kiti cha Urais wa CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan,amekipa heshima chama hicho na wanawake wote nchini kwani ameisimamia vyema ilani ya 2020-2025.
Hata hivyo amesema ,katika kipindi cha miaka mitano ijayo mbali na miradi itakayotekelezwa wilayani Kilwa pia watasimamia suala la amani,usalama na umoja wa nchi ambavyo ni kama mboni ya jicho la taifa.

“Amani, usalama na umoja huu ndio urithi wetu ambao viongozi wetu walituachia akiwemo Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere,nimefurahi nimemuona Nape Moses Nnauye na Kinjeketile Ngombale Mwiru, hawa baba zao wameshiriki kukijenga chama chetu na nchi,”amesema Dkt.Nchimbi.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako