December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

84 WAWEKWA KARANTINI TUNDUMA

NA MWANDISHI WETU

Katika kutekeleza maagizo ya serikali ya kuhakikisha wasafiri wote wanaotoka katika nchi zenye maambukizi Zaidi ya Virusi vya Corona wanatengwa, jumla ya wasafiri 84 kutoka Nchi ya Afrika Kusini wamewekwa karantini kwa muda wa siku 14 Katika halmashauri ya Mji wa Tunduma.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela ameyasema hayo alipofanya ukaguzi wa maandalizi ya utayari wa kupambana na Ugonjwa wa Virusi vya Corona  kwa Mkoa wa Songwe hususani maeneo ya Mipakani yaani katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na Halmashauri ya Mji wa Tunduma.