Na Mwandishi wetu, Timesmajira
JESHI la Polisi dawa za kulevya Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 13 wanao husika na kuuza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya ikiwemo bangi .
Watuhumiwa hao ni pamoja na Hamis Seif (18) Mkazi wa Mbondole na Bosco Bosco (18) Mkazi wa Kipunguni Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema Leo Juni 7, 2024 Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam SACP ,Muliro Muliro amesema watuhumiwa hao wamekamatwa na Puli 531 na kete 2,639 na misokoto 158 ambayo ilikuwa
tayari kutumiwa.
SACP Muliro amesema watuhumiwa hao pia walikuwa na viroba vinne vya bangi pia pikipiki mbili MC 673 CKM na MC 591 CUW zilizokuwa zinatumika kusambaza bangi hizo pia zimekamatwa.
“Jeshi la Polisi linaendelea kusimamia mkakati wake
maalum wa kuzuia vitendo vyote vya kihalifu katika jiji la Dar es Salaam. Kazi hii maalum ya
kuzuia vitendo vya kihalifu ni muendelezo wa kazi hiyo iliyoanza mwezi Aprili 2024 na inayoedelea kulenga, kufuatilia, kuchunguza na kukamata wahalifu mbalimbali pamoja na wanaopanga njama za kuiba, kuvunja nyumba, wanaouza, kusafirisha na kutumia dawa za kulevya”amesema SACP Muliro
Pia Jeshi hilo limemkamata
Hassan Yahya maarufu kama cobra na wenzake watatu ambao walikuwa wakitumia dawa za kulevya aina ya
bangi huku wakipanga njama za kufanya vitendo vya kihalifu yakiwemo makosa yaunyang’anyi.
Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Mei 21, 2024
maeneo ya Kipunguni B, Ukonga.
“Watuhumiwa hawa walikutwa na pistol toy 7, AK47 toy 2, Jambia toy 2, shoka toy 2, kama sehemu ya maandalizi ya kufanya kuhalifu”amesema
Na kuongeza kuwa”Jeshi la Polisi litaendelea kujikita katika kuzuia matukio ya kihalifu kwa kuafutilia kwa karibu makundi yote ya watu na hasa wanatumia dawa za kulevya na kufanya matukio ya kihalifu”amesema
Katika hatua nyingine Jeshi hilo la Polisi Kwa kipindi cha Aprili hadi Mei 2024 Jumla ya makosa 67 ya pikipiki yalikamatwa.
Amesema makosa hayo yalikuwa yakihusisha kutokuwa na leseni, kuzidisha abiria na kuendesha pikipiki wakiwa wamelewa ambapo madereva 21 walifikishwa mahakamani, na wengine walitozwa faini za papo hapo.
Madereva wa magari 6 walikamatwa kwa makosa ya kuendesha wakiwa wamelewa ambapo
madereva 2 walifikishwa mahakamani na wengine 4 walitozwa faini papo hapo.
Vilevile amesema katika kipindi cha mwezi Aprili hadi Mei 2024, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
salaam katika kusimamia mifumo ya haki jinai lilifanikiwa kupata matokeo Mahakamani ya
watuhumiwa mbalimbali.
Watuhumiwa hao ni pamoja na Agustino Daniel (22) Mkazi wa Vingunguti alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kulawiti kwenye Mahakama ya Wilaya Kinyerezi.
Conradi Nnkuru (43) mkazi wa Msongola kwenye Mahakama hiyo hiyo ya Kinyerezi
alihukumiwa miaka 30 jela kwa kosa la kubaka.
Unyang’anyi wa kutumia silaha washtakiwa 3 kwenye Mahakama ya Wilaya Temeke
walipata adhabu ya kifungo miaka 30 jela akiwemo Mikidadi Juma (40) mkazi wa Mbagala.
Aidha Jeshi hilo lilitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za kweli zitakazo pelekea kukamatwa kwa halifu haraka kabla hawajatekeleza
uhalifu wao.
Kwa upande wa usalama wa barabarani SACP Muliro amesema Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kuwafuatilia, kuwakamata na kuwafikishwa mahakamani madereva wasiotii
sheria na kanuni za usalama barabarani wakiwemo walevi na makosa hatarishi ya wapanda
pikipiki za miguu miwili na miguu mitatu.
More Stories
Balozi Nchimbi kuongoza waombolezaji mazishi ya Kibiti leo
Dkt.Tulia,apewa tano kuwezesha wananchi
Nkasi yajipanga kukusanya mapatoÂ