January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

10 mbaroni tuhuma za mauaji ya mlinzi

Judith Ferdinand,Timesmajira Online, Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mlinzi aliyefahamika kwa jina la Yumen Elias(54) mkazi wa Nyashishi wilayani Nyamagana mkoani hapa.

Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa katika tukio hilo lilitokea Januari 16,2024 majira saa 03:00 usiku eneo la Mwananchi, Kata ya Mahina, Wilaya ya Nyamagana ambapo kuliripotiwa tukio la kuuwawa kwa Yumen Elias(54) mlinzi na mkazi wa Nyashishi.

Ambapo inadaiwa kuwa aliuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani na baada ya taarifa hiyo kuripotiwa kituo cha Polisi Nyakato,jeshi hilo lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa kumi waliohusika katika mauaji hayo.

Mutafungwa ameeleza kuwa ilipofika Januari 18,2024 kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti mkoani Mwanza Askari Polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao ambao ni Julias Joseph kwa jina maarufu Bwashee (22), mkazi wa Igoma,Paul John(23) kwa jina maarufu Doyi, mkazi wa Mwananchi.

Wengine ni Leonidas Juma(19),Bukwimba, kwa jina maarufu wa Dar es salaam, , mkazi wa Buhongwa,Abdallah Hassan kwajina maarufu Dula(31) mkazi wa Nundu,Edward Bonface (19) mkazi wa Mahina,Mussa Robart (22) fundi magari, mkazi wa Ilemela Kanisani,Steven Emmanuel(18)mkazi wa Nyakato Sokoni.

Pia George Mang’era Koloso(50) mfanyabiashara, mkazi wa Nyegezi,Hamis Omary maarufu mlangwa (21) mfanyabiashara, mkazi wa Mabatini na Charles Chacha maarufu Ryoba(27) mkazi wa Mahina Kati, waliohusika na mauaji ya mlinzi huyo.

Ambapo upelelezi unakamilishwa mara moja na watuhumiwa watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.