March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zungu:Jimbo la ilala kuadhimisha siku ya Samia Oktoba 29

Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)

MGOMBEA UBUNGE JIMBO la Ilala Mkoani Dar Mussa Zungu, amesema ifikapo October 29 mwaka huu jimbo la Ilala kuadhimisha siku ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ijulikanayo SAMIA DAY.

Mussa Zungu amesema hayo jimbo la Ilala wakati wa mapokezi ya mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Emanuel Nchimbi alipowasili wilaya ya Ilala.

“Siku ya Simba day tayari tumeazimisha ,Yanga Day nayo tumeadhimisha sasa ifikapo October 29 Jimbo la Ilala wote ni madhimisho ya Dkt.Samia DAY kwenda kupiga kura ya chama cha Mapinduzi CCM”amesema Zungu.

Zungu amesema Dkt samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika nchi yetu hivyo siku hiyo ya October 29 Mwaka huu zawadi yake kubwa ni kupiga kura ya chama cha Mapinduzi.