December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zungu awataka vijana kujikwamua kiuchumi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu, amewataka vijana nchini kujikwamua kiuchumi kataka kufanya kazi na kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluhu Hassan katika kukuza Uchumi .

Naibu Spika Mussa Zungu alitoa agizo hilo kwa Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Taasisi ya AMO Foundation.

“Vijana sio lele mama ,ujana sio kujirusha ,ujana kujiamini na kufanya kazi za kujikwamua kiuchumi katika kujenga Taifa letu na kuunga mkono Juhudi za Rais za kukuza Uchumi wa nchi ” alisema Zungu .

Naibu Spika Mussa Zungu alipongeza Taasisi ya AMO Foundation katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuwaunganisha vijana pamoja kuwapa Elimu na fursa za uchumi Ili waweze kujikwamua kiuchumiAliwataka vijana kuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Ili Taifa letu liweze kusonga mbele amewataka vijana watafakari wasipotoshe Umma katika kujenga nchi .

Aidha Zungu alisema sasa hivi ni kipindi cha kufanya kazi sio cha vita hivyo vijana wa kitanzania amewataka wafanye kazi ya kujenga nchi wazazi wao wameteseka katika kuwatafutia Elimu na wamewasomesha Ili waweze kuwa viongozi bora wa Taifa .

Wakati huo huo Naibu Spika Zungu alitoa hofa vijana watano kusoma bure kozi ya (TEHAMA) Ili waweze kuwa Wataalam bora katika nyanja ya Sayansi na teknolojiaMkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema Rais Dkt.Samia Suluhu Haasan, anawajibika katika miradi mikubwa ya Maendeleo ya kujenga uchumi wa nchi kla siku kwa ajili ya kukuza Uchumi wa nchi.

Alisema uwajibikaji wa Vijana unatakiwa uanze mwenyewe katika familia kwa kuweka safi Mazingira ya nyumbani kwako .

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo aliwaasa vijana wawajibike kufanya kazi Ili kukuza Uchumi katika kuunga mkono Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DktSamia Suluhu Hassan katika kujenga Tanzania ya Uchumi wa viwanda .

Mkurugenzi wa Taasisi ya AMO Foundation Amina Good alisema Kongomano la vijana ni kampeni Maalum ya kuwasaidia vijana katika kupata Elimu ya. Ujasiriamali katika kuwawezesha vijana .

Mkurugenzi wa AMO Foundation Amina alisema katika Kampeni hiyo wameanza na vijana 50 malengo makuu kuwawezesha vijana wajikwamue kiuchumi wakiwemo wao na familia zao .

Alisema vijana hao waliowapa Elimu wakiwapa vifaa watakuwa wanawafatilia kuangalia maendeleo yao ikiwemo pia kuwa fungulia akaunti Benki na kuwatafutia masoko .Mwisho