January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zuchu afungiwa kuimba Mziki

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

BARAZA la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, ( BASSFU), limemfungia msanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu kwa jina la Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita.

Aidha BASSFU pia limepiga marufuku redio na televisheni za visiwani humo kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi hicho.

Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la hivi karibuni Zuchu akiwa jukwaani kwenye Tamasha la Full Moon Party akitumbuiza na alitoa matamshi na kuonesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya Kinzanzibari.

Aidha alijitapa kwa madaha stejini kwa kuimba kuwa wanawake wote wanaommendea mwanaume wake kamwe hawawezi kumtoa mikononi mwake hata wakimpa kinyume na maumbile huku akionesha kwa ishara.

Baada ya tamko hilo, Zuchu ameandika barua ya kuomba radhi kwa BASSFU pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) huku akielezea kuwa nia yake ilikuwa njema ya kutaka kutoa burudani na furaha kwa mashabiki wake.