December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziwa Nyasa kuanza kuwa chanzo kikuu cha maji

Na Esther Macha Timesmajira Online, Kyela

NAIBU Waziri wa Maji (Mb) Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa wizara ya maji katika mipango yao ya muda mrefu wameanza kutumia katika miradi ya maji ziwa Nyasa kuwa chanzo kikuu cha maji endelevu na kuja kutumia kwenye miradi mikubwa ya maji .

Mhandisi Mahundi amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya Ziwa Nyasa kuwa chanzo kikuu cha maji Wilayani Kyela Mkoani Mbeya.

“Sisi wanawake tumekutana hapa Fukwe ya Ziwa Nyasa kwa kujadili masuala mbali mbali ya kiuchumi ,tumefika hapa kufanya siasa zetu lakini pia tumeona pia fursa za Ziwa hili ambapo kitakuwa chanzo kikuu cha maji kwa Tanzania na Malawi hivyo ni Neema kubwa kwa Tanzania na Malawi “amesema.

Amesema Ziwa Nyasa nje ya kulitumia kama kivutio kuwa ni Fukwe kama wizara katika mipango yao ya muda mrefu kulitumia katika miradi yao ya maji na tayari wameanza kufanya tafiti mbali mbali za kuona namna gani wanalitumia Ziwa hilo na miradi midogo midogo wameanza kutumia kupata maji kama chanzo.

“Na hili Ziwa Nyasa ni ziwa ambalo nchi ya Malawi wanatumiia na kuwa mwaka 2021, Waziri wa Maji Jumaa Aweso aliweza kushiriki kikao Malawi na kujadili masuala mbali mbali kuona namna njema kufanya Ziwa hilo kuwa endelevu na wamekubaliana kuja kujenga Bwawa kubwa kwenye mpaka wa Malawi na Kyela Tanzania na hata ofisi inayoendesha mkataba wa Malawi na Tanzania ipo Wilaya ya Kyela,kwa hiyo tutaendelea kushirikiana na Malawi kuona Ziwa hili linatumika vizuri kwa watanzania wote”amesema Mhandisi Mahundi.

Mkuu wa wilaya ya Kyela mkoani Mbeya Josephine Manase amesema kuwa uwepo wa Ziwa Nyasa utakuwa fursa kubwa kwa kuwa chanzo kikuu cha maji kwa nchi mbili Tanzania na Malawi.