November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ziara ya Rais Samia ni Non Stop kuzindua miradi mikubwa ya maendeleo

-Akataa daraja kupewa jina lake na kupendekeza heshima hiyo apewe Mama Maria Nyerere kutambua mchango wake kwa Baba wa Taifa katika kupibania Uhuru wan chi yetu.

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara ya kikazi ndani ya mkoa wa Rukwa kwa siku ya leo kwa kuzindua mbalimbali ya maendeleo na kupokelewa kwa kishindo na wakazi wa Sumbawanga.

Awali Rais Samia alizindua jengo la ofisi za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kalambo ambalo limegharimu zaidi ya shilingi billion 5 za kitanzania kisha kufuatiwa na uzinduzi wa Barabara ya Sumbawanga-Matai-Katanga yenye urefu wa kilometa 107.14 anabyoimegharimu jumla ya shilingi bilioni 105 barabara hiyo itasaidia kurahisisha usafiri na uchukuzi ambapo hapo awali ilitumika siku nzima wananchi kusafiri kupata huduma maeneo yanayounganishwa na barabara hiyo.

Rais Samia pia alipata wasaa wasaa wa kuzungumza na maelfu ya wakazi wa kalambo waliojitokeza kumlaki katika ziara hiyo alipokuwa anafungua barabara hiyo ya Sumbawanga, matai na kisanga na kuwahakikishia Wananchi kuwa serikali itaendelea kufanya jitihada kuhakikisha huduma muhimu zinaboreshwa kwa ajili ya ustawi wa jamii nzima.

Vilevile Rais Samia amezindua Vihenge , maghala ya kuhifadhi chakula ya NFRA na msimu wa ununuzi wa nafaka eneo la konondo Halmashauri ya Sumawanga mradi huo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 14 katika hafla hiyo Rais Samia amewasihi Wananchi kuchangamkia fursa za kuzalisha kwa wingiili mazao yapate masoko nje ya nchi kupitia NFRA.

Katika ziara hiyo Rais Samia ameweka jiwe la msingi kuashiria ufunguzi wa Chuo cha VETA Sumbawanga pamoja na kupata wasaa kuwasikiliza wanafunzi wa chuo hicho wa fani mbalimbali ambao walimshukuru Rais Samia kwa uwekezaji unaowapa matumaini kuzikabbili changamoto za maisha.

Kubwa zaidi ni uwekaji wa jiwe ka msingi katika uwanja wa ndege wa Rukwa utakaofungua uchumi wa Mkoa wa Rukwa pamoja uzinduzi wa chuo cha Ualimu Sumbawanga akizungumza katika ufunguzi wa chuo cha Ualimu Rais Samia amewashukuru Walimu kwa kazi kubwa ya thamani wanayoifanya ya kufundisha na kuwaomba kuchapa kazi kwani kazi wanayoifanya ni sadaka inayoendelea.