December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zaidi ya watu 30 kutoka jiji la Hamburg kuwasili Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu,timesmajira, online

ZAIDI ya ujumbe wa  watu 30  kutoka katika Jiji la Hamburg nchini Ujerumani wanatarajia kuwasili Dar es Salaam  kwa lengo la kuadhimisha miaka 12 ya uhusiano wa Miji Dada kati ya Jiji la Dar es Salaam na Jiji la Hamburg ulioanzishwa tangu mwaka  2010.

Pia Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kwa wiki katika sherehe za kuadhimisha mahusiano hayo ya Majiji mawili Julai 3,2022 katika viwanja vya mnazi mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa  Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amesema maadhimisho hayo yanatarajia kuanzia rasmi  Juni 30,20222 hadi Julai 3,mwaka huu yakiambatana na matukio mbalimbali.

Amesema katika maadhimisho hayo pande hizi mbili za miji  zitasherehekea mafanikio waliyofikia hadi sasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi,afya,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,utamaduni,michezo,elimu,stadi za kazi za wanawake,vijana na watu wenye mahitaji maalum.

”Awali maadhimisho haya yalipangwa kufanyika mwaka 2020 lakini ilishindikana kutokana na janga la UVIKO-19,katika maadhimisho haya pande hizo mbili zitasherekea mafanikio waliyofikia tangu kuanzishwa kwa uhusiano wao,”amesema

Aidha amesema Julai mosi 2022,viongozi wa miji hiyo miwili watasaini makubaliano ya kudumisha uhusiano huo kwa kutoa nafasi kwa wadau wengi zaidi kunufaika na fursa zinazojitokeza kupitia uhusiano huo.

“Sherehe za maadhimisho ya uhusiano huu zitafanyika siku ya jumapili Julai3,2022 katika viwanja vya mnazi mmoja hivyo tunaomba wananchi wajitokeze kushiriki na kutumia fursa hiyo kwa manufaa ya Jiji la Dar es Salaam,”amesema