March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yas, Mixx kuendelea kutoa huduma bora kwa Wateja

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

DUNIA ikiwa inaadhimisha wiki ya Kimataifa ya huduma kwa wateja, watoaji huduma nchini, wametakiwa kuzingatia viwango vizuri vya huduma wanazozitoa zikizingatia misingi ya ubora ili kufanya biashara zao kuwa endelevu.

Rai hiyo ilitolewa Jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja kutoka kampuni ya Yas na Mixx By Yas.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Yas, Pierre Canton Bacara amewataka watoaji huduma wa kampuni hizo mbili kuzingatia ubora katika kuwadumia wateja.

“Kwanza wateja wetu milioni 26 kote Tanzania, asanteni sana kwani mmeifanya Yas kuwa sehemu ya maisha yako, hivyo hatuna budi kujivunia kukuhudumia.

“Tunakuona, tunakuthamini, na tunaahidi kuendelea kukupa huduma bora zaidi, kila siku,” amesema Pierre Canton Bacara

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx By Yas, Angelica Pesha amesema Mixx inajivunia zaidi ya miaka 15 ya ukuaji, ubunifu, na huduma za kidijitali zinazogusa maisha ya Watanzania.

Amesema, Kaulimbiu ya mwaka huu, “Mission: Possible,” ambayo inakumbusha kwamba hakuna changamoto isiyoweza kushindwa wakimweka mteja mbele.

“Kwa Mixx, “Mission: Possible” ina maana ya kubadili changamoto za wateja wetu kuwa fursa; fursa za kuboresha maisha yao, kurahisisha miamala, na kuwaunganisha na ulimwengu wa kifedha kidijitali,” amesema Angelica Pesha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa huduma kwa wateja, Mwangaza Matotola amesema katika wiki hii wanasherekea jitihada za watoa huduma zaidi ya elfu moja wanaohudumia wateja zaidi ya milioni 26.