Na Jackline Martin
Kufuatia siku ya Sayari Duniani ambayo huadhimishwa kila tarehe 22 Aprili, Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kwa kushirikiana na Chuo Cha Usatwi wa Jamii wameungana kwa pamoja katika kuendeleza Kampeni ya ‘Soma na Mti,’ ambapo kwa mwaka huu Kampeni yao ni ‘wekeza katika Dunia’ lengo ni kuwawezesha vijana kuhifadhi sayari kwa kupanda miti 100.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa upandaji wa miti chuoni hapo, Meneja Mawasiliano WWF Tanzania Joan Itanisa amesema Kampeni hiyo ni muendelezo wa kuungwa mkono Kampeni ambayo ilianzishwa na ofisi ya Makamu wa Rais chini ya Waziri Seleman jafo ya ‘Soma na Mti’ ambapo mpaka sasa wamefikisha miti elf 10 na Kwa kipindi hiki Cha mvua wanampango wa kufikisha miti Milioni tatu kwa kuanzia;
“Huu ni muendelezo wetu wa kuungwa mkono Kampeni ambayo ilianzishwa na ofisi ya makamu wa Raisi chini ya Waziri Seleman jafo ya ‘Soma na Mti’ ambapo inaelekeza kwamba kila mwanafunzi Tanzania kuanzia shule ya msingi mpaka chuo kikuu anapanda walau mti mmoja lakini sisi tunasema hatuishii kupanda tu anapanda mti lakini anahakikisha kuwa anapokuwa shuleni anautunza mti ule”
Aidha Itanisa amesema Waziri jafo analengo la kupanda miti Milioni 14 kwa kila shule na chuo nchini Tanzania, hivyo kutokana na yeye kuwakabidhi WWF Kampeni hiyo watahakikisha kwamba wanafikia lengo hilo kadri inavyowezekana.
Itanisa alisema wanategemea wadau wengine pia wataungana nao ili kuweza kuhakikisha kwamba Kampeni hiyo ya Soma na Mti inafanikiwa na kila mwanafunzi Tanzania anakuwa na Mti wake.
Kwa upande wake Mshauri wa wanafunzi chuo Cha Ustawi Dkt. Andrew Randa amesema kutokana na Dunia ya leo kukumbwa na tatizo la mazingira inayopelekea uchafuzi wa Hali ya hewa na sehemu mbalimbali kuharibika, kwa miaka mitano ijayo wanatarajia kwamba zoezi hili la upandaji miti matokeo yake yataonekana kwa kuleta Suluhu ya tatizo hilo la mazingira
Amesema Zoezi hilo la upandaji miti lisiwe tu kwa Taasisi ya ustawi wa Jamii bali na Kwa vyuo vingine kuendeleza zoezi hilo ili kuhakikisha wanalinda sayari ya dunia.
Naye Mwanafunzi wa chuo Cha ustawi, Mickdad Uhuru amesema wananafurahi kuungana na WWF katika kushiriki zoezi hilo la kupanda miti lakini pia ametoa wito kwa wanafunzi wote kuunga mkono Kampeni hiyo vilevile waendelee kuitunza miti hiyo.
More Stories
Mwabukusi akemea wanasiasa wanaotoa kauli za kibaguzi kuelekea uchaguzi mkuu
TAA yatakiwa kulipia mirabaha inayohusiana na matumizi ya muziki katika viwanja vya ndege nchini
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yafanya ziara ya kujifunza uongezaji thamani wa madini nchini Zambia