Na Joyce Kasiki,Timesamajira online,Dodoma
MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Vipimo (WMA) Stella Kahwa amesema katika kipindi cha miaka mitano taasisi hiyo imechangia zaidi ya shilingi bilioni 24 katika pato la Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mikakati ya taasisi hiyo kwa mwaka 2023/24,Mtendaji mkuu huyo amesema hayo ni mafanikio makubwa.
Amesema katika utekelezaji wa majukumu yake WMA imeendelea kutoa mchango katika kuchochea maendeleo ya sekta za kiuchumi na kijamii nchini,kuchochea uzalishaji wa bidhaa unaozingatia vipimo sahihi,kuendelea kuchangia katika mfuko huo Mkuu wa Serikali.
Aidha ametoa mchanganuo kwa namna ambavyo wakala huo umekuwa ukichangia ambapo 2018 /19 Wakala umechangia shilingi bilioni 4.0,2019/20 shilingi bilioni 5.3,2020/21 shilingi bilioni 6.4,2021/22 shilingi bilioni 4.1 na 2022/23 shilingi bilioni 4.3.
Kuhusu majukumu ya taasisi hiyo amesema ni pamoja na kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye sekta za Biashara ,Afya,Usalama na Mazingira ili kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matokeo ya upimaji usio sahihi katika maeneo hayo na kuhifadhi vipimo vyenye usahihi wa ngazi ya kati na kuhakikisha usahihi wake unakubalika na vile vya kimataifa.
Majukumu mengine ni kusimamia matumizi ya sahihi ya vipimo,kukagua na kuhakiki bidhaa zilizofungashwa kuidhinisha aina mpya ya vipimo vinavyoingizwa toka je ya nchi na vinavyoundwa hapa nchini.
Vile vile amesema majukumu mengine ni kutoa ushauri wa kitaalam kuhusiana na vipimo kwa serikali ,Mashirika ,Taasisi na wadau wengine na kutoa vibali vya ugenzi na leseni za ufundi na uundaji wa vipimo mbalimbali.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato