January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Kilimo yatoa darasa la sumukuvu kwa Wahariri

Na Joyce Kasiki,Timesmajira Online, Dodoma

WIZARA ya Kilimo kupitia mradi wake wake wa kudhibiti sumukuvu (TANPAC) imewakutanisha wahariri wa vyombo mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia semina ya udhibiti wa sumukuvu kwa lengo la kuelimisha jamii.

Akizungumza katika semina hiyo, Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti sumukuvu Clepin Josehat amesema tatizo la sumukuvu hapa nchini Tanzania limeanza 2016 katika Mkoa wa Dodoma.

Amesema Malengo ya Mradi huo ni pamoja na mambo mengine ni kuimarisha usalama wa chakula haha nchini , kuimarisha uchumi wa nchi kupitia mauzo ya chakula nje ya nchi pamoja na kuimarisha Afya ya jamii.

Aidha Clepin amesema Ili kufikia Malengo hayo mradi huo unajenga miundombinu ya msingi katika kudhibiti sumukuvu lakini pia umelenga kuimarisha taasisi za udhibiti na utafiti Ili udhibiti wa sumukuvu iwe endelevu.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu Huria Dkt. Happy Magoha amesema elimu kuhusu usalama wa chakula inatakiwa kutolewa mara kwa mara,ili kuepuka mazao kupata Sumu Kuvu ikiwemo kuepusha madhara kwa jamii.

Amesema elimu hiyo inatakiwa kutolewa kwa jamii mara kwa mara ili kuhakikisha jamii inatambua umuhimu wa kuhifadhi vizuri mazao ili yasipate Sumu Kuvu ambayo ina madhara kwao.