Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
KATIBU MKuu Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Dkt.Jimmy Yonazi amesema Tanzania imekusudia kufungua ajira kwa watanzania kitaifa na kimataifa ili kuwa nchi yenye fursa nyingi za uchumi wa kidigitali ili nchi zingine zije kujifunza.
Dkt.Yonazi amesema hayo jijini hapa leo katika kikao kazi cha uchambuzi wa fursa za kiuchumi za sekta ya mawasiliano Kitaifa na Kimataifa ambapo amesema ili Tanzania iwe nchi yenye fursa lazima wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano waongeze juhudi katika kukuza maarifa na yatakayokuza uchumi shindani wa kidijitali ili kuwa kitovu cha watu kujifunza namna ya kutafuta fursa katika taasisi za kimataifa.
Hivyo amesema ili kuifanya Tanzania kuwa nchi ya fursa lazima kila mfanyakazi wa sekta hiyo ailewe sekta hiyo na mifumo yake ili iwe rahisi kuifanyiakazi.
“Kila mmoja atambue jukumu lake na siyo kuja ofisini na kurudi nyumbani tu kwasababu kufanya hivyo siyo kufanyakazi bali ni kwenda kazini tu kitendo ambacho akileti maendeleo wala fursa yoyote kwasababu hizi fursa zinatafutwa.
Aidha amesema ili nchi ipige hatua kimataifa lazima watendaji wake watambue mahitaji ya nchi kabla ya uhitaji wa mahitaji hayo kwasababu upatikanaji wake unakua mgumu na mwisho mambo yanashindwa kutekelezeka kwa usahihi na ubora unaohitajika.
“Kwamfano sasa hivi tunaelekea kwenye suala la sensa na tunaenda kutumia vishikwambi na vitahitajika vingi tusipojua mapema wapi tutavipata tutaenda kule China tutaangaika kwenye makampuni yanayotengeneza huku muda ukiwa umeisha hatutapata vyenye ubora hivyo tujitahidi kujua mapema mahitaji yetu kabla,”amesema.
“Zinatokeaga kazi za mataifa mengine je huwa mnaomba ilimfanyekazi huko mpate uzoefu wenzetu wanavyofanya ili iwefursa na kwetu pindi tunapotaka kujifunza juu ya fursa za mataifa mengine,”ameuliza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari, Mulembwa Munaku amesema kuwa watatekeleza maagizo ya serikali ili kuongza ajira pamoja na pato la Taifa.
“Wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari Dira yake ni kuwa idara imara iliyosambaa nchini kote yenye wataalam waliobobea na wenye uwezo wa kutoa huduma ya mawasiliano na habari zilizo sahihi na zenye kuaminika,”amesema.
More Stories
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili
ACT-Wazalendo,waitaka Polisi kutobeba chama kimoja